Jump to content

User talk:MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE

Page contents not supported in other languages.
From Wikipedia, the free encyclopedia

KUNENA KWA LUGHA

KUNENA KWA LUGHA

[edit]

KUNENA KWA LUGHA: . . .

Jina la Bwana lipewe sifa kaka na dada katika Kristo Yesu;. KARIBU MPENDWA KWA SOMO HILI ZURI LA KUNENA KWA LUGHA. Kwa neema ya Mungu napenda tutafakari somo linalohusu kunena kwa Lugha: Mara nyingi kumekuwa na mizozo kati ya muumini na muumini, na kati ya dhehebu na dhehebu juu ya kunena kwa lugha. Yako baadhi ya makanisa muumini asiponena kwa Lugha anaambiwa hana Roho mtakatifu, na hivyo imewapelekea baadhi ya watu kukata tamaa hata ya kusali kisa kaambiwa hana Roho Mtakatifu kwa sababu Haneni kwa Lugha, Jambo ambalo si kweli kwamba mtu asiponena kwa lugha hana Roho Matakatifu, Huo ni uwongo tu. Nini maana ya LUGHA? LUGHA: ni mpangilio wa maneno yenye kuleta maana kwa mzungumzaji na msikilizaji. Ina maana kwamba ikiwa mtu ananena maneno lakini hayaleti maana yoyote hiyo sio Lugha bali ni machafuko. 1 Wakorintho 14:10-11 "Yamkini ziko sauti za namna nyingi duniani, wala hakuna moja isiyo na maana. Basi nisipoijua maana ya ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye; naye anenaye atakuwa mjinga kwangu." Kwa hiyo Lugha sahihi ni lazima ilete maana. KUNENA KWA LUGHA, ni kutamka maneno ambayo ni mageni/ mapya kwa mzungumzaji au kwa msikilizaji Au ni kuzungumza lugha yoyote ambayo ni ngeni kwa mzungumzaji au msikilizaji. CHIMBUKO LA KUNENA KWA LUGHA: Zamani hakukuwa na makabila kama ilivyo siku hizi, Lakini tunapata chanzo cha makabila katika kitabu cha mwanzo sura ya 11, wakati watu walipojenga mnara wa Baberi, na Mungu ili kuzuia ule uasi ikabidi achafue lugha yao na washindwe kuelewana: Mwanzo 11:7 "Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao." Mwanzo 11:9 "Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote." Kwa hiyo kunena kwa Lugha pia inaweza ikawa ni Machafuko, pindi endapo kuna kuwa hakuna utaratibu maalumu wa kunena au kukosa maelewano katika unenaji wa lugha: 1 Wakorintho 14:27 "Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri." 1 Wakorintho 14:33 "Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu." Na ndio maana Paulo anasema; 1 Wakorintho 14:23 "Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu?" Sasa wapo watu hunena lugha ambazo hazieleweki kwa wasikilizaji na pia wao wenyewe hawajui wananena nini, ukiwauliza wanadai kwamba hizo ni lugha za Malaika ambazo hata shetani hajui:Ukweli ni kwamba Hakuna lugha ambayo shetani haifahamu na pia tukumbuke kwamba Shetani kabla ya kuanguka alikuwa ni kiongozi wa Malaika Mbinguni na hivyo anafahamu kila kitu. Kwa hiyo hauwezi ukamficha shetani lugha yoyote. Na ikiwa lugha hizo zinazonenwa ni lugha za Malaika mbona hatuoni manabii wa zamani wakinena kwa Lugha walipotokewa na malaika? Au Yesu mwenyewe mbona hatuoni mahali popote akinena hizo lugha za malaika? AINA ZA KUNENA KWA LUGHA: Zipo aina tatu za Kunena kwa Lugha: 1. NI KUNENA KWA LUGHA PASIPO KUTOA MANENO: Mfano: Mpo watu kadhaa mahali na mmoja wenu inabidi aombee chakula, Lani yeye hatoi sauti bali anaomba kwa moyoni: Huko ni kunena kwa lugha maana wengine hawaelewi nini kilichoombwa, ijapokuwa muombaji anajua alichokiomba, hapo anakuwa amejifaidisha mwenyewe: 1 Wakorintho 14:2 "Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake." 1 Wakorintho 14:16 " Kwa maana wewe ukibariki kwa roho, yeye aketiye katika mahali pa mjinga ataitikaje, Amina, baada ya kushukuru kwako, akiwa hayajui usemayo?" Mfano mwingine ni: Hana wakati alipokuwa anamuomba Mungu apate mtoto, alikuwa akiomba kwa moyo pasipo kutamka maneno bali mdomo ulikuwa ukichezacheza, mpaka Eli akasema Hana amelewa: 1 Samweli 1:13-15 "Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa. Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai yako. Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za Bwana." Mfano: Hana angekuwa mtu mwingine angeweza kumjibu vibaya Eli, kwa kuambiwa kwamba amelewa, wakati yeye anaomba, na matokeo yake yangetokea machafuko. 2. KUNENA KWA LUGHA KWA SAUTI: Aina hii ya kunena kwa lugha ni kuzungumza/kuomba kwa lugha yoyote ambayo ni ngeni kwa mzungumzaji au msikilizaji. Aina hii ya kunena kwa Lugha ndio ambayo wakati Fulani inahitaji mtu wa kutafsiri ili kila mtu aliyepo aelewe ni nini Kilichonenwa/kuombwa. 1 Wakorintho 14:27-28 "Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri. Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu." NOTE: Kanisa la Korinto lilikuwa ni kanisa lililokuwa linakusanya waumini wa mataifa mbalimbali, kwa sababu Korintho ulikuwa ni mji wa biashara, na hivyo waumini wa Mataifa mbalimbali walipokuwa wakikusanyika Kanisani kwa ajili ya ibada kila mtu alitaka atumie lugha yake kwenye ibada aidha katika kuhubiri au katika kuomba, na hivyo Paulo anawaonya kwamba ikiwa kuna mtu anataka kutumia lugha yake kunena na kanisa, basi ahakikishe yupo mtu atakaye tafsiri hiyo lugha yake kwa watu wengine, lakini kama hakuna mtu wa kumtafsiria basi atulie tu asinene lolote. 3. KUNENA KWA LUGHA NGENI ISIYO YAKO: Ieleweke kwamba aina ya kwanza na ya pili ya kunena kwa lugha: mnenaji anakuwa anafahamu ni nini anachokinena, bali changamoto inakuwa kwa wasikilizaji, ndio wanakuwa hawaelewi kinachonenwa. Lakini aina hii ya 3 ya kunena kwa Lugha ni kwamba Mnenaji ananena Lugha isiyokuwa yake. Mara nyingi mfumo huu wa kunena kwa Lugha unatokea kwa Nadra na kwa kusudi maalumu, hasa katika kupeleka Injili katika maeneo ya Ugenini: Mfano: Ni kile kilichotokea siku ya Pentekoste, Mitume walikuwa Wagalilaya na walipokutanika Walitumia Lugha yao, Lakini wasikilizaji kila mtu aliwasikia mitume wakinena kwa Lugha zao. Ina maana kwamba Roho mtakatifu alikuwa anamtafsiria kila mtu kwa lugha yake mwenyewe: Matendo ya Mitume 2:6-8 "Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?" Hivyo lugha zilizonenwa siku ya Pentekoste zilikuwa ni lugha za Mataifa mengine. Ina maana kwamba siku hiyo Kama wewe ni Mchaga ungekuwepo ungesikia mitume wakinena Kichaga, Kama wewe ni Msukuma ungewasikia mitume wakinena Kisukuma, kama wewe ni mnyakyusa Ungewasikia mitume wakinena Kinyakyusa NK. Kwa hiyo wale ndugu mnaotumia Matendo 2 kutetea unenaji wa lugha zisizojulikana mnakosea, Maana lugha walizonena mitume zilijulikana. KUSUDIO LA KUNENA KWA LUGHA: Yesu wakati anaondoka aliwaambia wanafunzi wake kwamba: Marko 16:17 "Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya." Ahadi hii Yesu aliitoa baada ya kufufuka, kwamba Wanafunzi wake watasema kwa lugha mpya. Sasa baadhi ya watu hutumia fungu hili kwa kudai kwamba lugha mpya ni Lugha isiyojulikana, Si kweli, maana Ahadi hii ndio ilikuja kutimizwa katika Matendo sura ya 2. Anaposema watasema lugha mpya ina maana gani? Ina maana kwamba Lugha watakazo sema mitume ni Lugha za watu wa Mataifa ya hapahapa Duniani, lakini kwao zitakuwa mpya kwa sababu ndio mara yao ya kwanza kwao kuzinena. : Ina maana kwamba ukisikia lugha yoyote inazungumzwa isiyokuwa ya kwako hiyo ni ngeni kwako au ni mpya, kwa sababu ndio mara yako ya kwanza kuisikia au kuinena. Je, wao mitume lugha walizosema zilikuwa kweli mpya kabisa hazijulikani Duniani? Matendo ya Mitume 2:4-8 "Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?" Ahadi ya Yesu katika Marko 16:17 ndio ilitimizwa hapo, na hapo anasema ; wakaanza kusema kwa lugha nyingine, hizi lugha nyingine ndiyo lugha mpya, ambazo zilikuwa ni lugha za watu wa Mataifa mengine: Kusudi la Mungu kuruhusu kunena kwa lugha sio kwa ajili ya maburudisho ndani ya Makanisa, bali aliruhusu kunena kwa Lugha kwa kusudi moja tu, la kueneza Injili, Maana Yesu alisema. Mathayo 28:19 "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu" Sasa haingekuwa rahisi Mitume kuzunguka kila mahali kueneza injili, alicho kifanya Mungu aliyakusanya Mataifa kutoka kila kona ya Dunia ili kila atakayesikia injili akaieneze katika Taifa lake. Na hivyo kusudi kubwa la kunena kwa lugha ilikuwa ni kueneza Injili kwa mataifa yote. Maana siku ile ya Pentekoste kulikuwa na Mataifa kutoka kila kona ya Dunia. Matendo 2:5 inasema: "Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu." Matendo ya Mitume 2:9-13 "Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia, Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya? Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya." Kwa hiyo kupitia muujiza huu wa kunena kwa lugha Injili ikafika kila kona ya Dunia. Baadaye Kanisa la Korintho walianza kunena kwa lugha kama sehemu ya utaratibu wa Ibada kwa kuiga kile kilichofanyika siku ya Pentekoste, na Paulo akawaonya; 1 Wakorintho 14:20-21 "Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima. Imeandikwa katika torati, Nitasema na watu hawa kwa watu wa lugha nyingine, na kwa midomo ya wageni, wala hata hivyo hawatanisikia, asema Bwana." Kwa hiyo kilichotokea siku ya Pentekoste ulikuwa ni kutimizwa kwa Utabiri wa kupeleka injili kwa mataifa yote, Lakini Paulo anawaambia pia Kunena kwa Lugha ni Ishara kwa wasioamini: 1 Wakorintho 14:22 "Basi, hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini lakini kuhutubu si kwa ajili yao wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio." Ina maana kwamba hata siku ya Pentekoste kilichowafanya mataifa wamsikilize Petro ni kwa sababu walitekewa baada ya kuwaona wagalilaya wakizungumza lugha zao. Na kupitia ishara hii ya kunena kwa lugha wakabatizwa watu 3000, maana walisikia habari njema kila mtu kwa lugha yake. NOTE: Matukio yote ya kunena kwa lugha yalihusisha upelekaji wa injili kwa watu wa Mataifa, 1. Matendo 2:1-12, kulikuwa na watu wa Mataifa. 2. Matendo 10:44-47, kulikuwa na watu wa Mataifa kwa Kornelio. 3. Matendo 19:1-6, Kulikuwa na watu wa Mataifa pale Korintho. Hakuna mahali mitume walinena kwa Lugha kama sehemu ya Utaratibu wa Ibada, bali kunena kwa lugha kulitumika katika upelekaji wa injili kwa mataifa ili iwe Ishara ya watu kumjua Mungu pindi wanaposikia lugha tofauti zikinenwa. Kwa hiyo baada ya Kanisa la Korintho kuanza machafuko ya kunena ovyo kwa Lugha Paulo ikabidi awakemee na kuwapa utarabu mzuri, Na niwaombe wale ndugu zangu mnaopenda kunena kwa lugha bila utaratibu, mfuate utaratibu huu, na ikiwa hamfuti hayo ni machafuko ndani ya kanisa. 1. Kila lugha inayonenwa ni lazima ilete maana; 1 Wakorintho 14:7-8 "Hata vitu visivyo na uhai vitoapo sauti, ikiwa ni filimbi, ikiwa ni kinubi, visipotoa sauti zilizo na tofauti, itatambulikanaje ni wimbo gani unaopigwa kwa filimbi au kwa kinubi? Kwa maana baragumu ikitoa sauti isiyojulikana, ni nani atakayejifanya tayari kwa vita?" Je, lugha zinazonenwa siku hizi makanisani zina maana gani? 2. Anayenena kwa Lugha ni lazima akili yake ifahamu ananena nini. 1 Wakorintho 14:14-15 "Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda. Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; mtaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia." Je, ni kweli mnaponena akili zenu zinafahamu ulichokuwa ukikinena, au ukimaliza kunena hukumbuki ulichokinena? Ikiwa akili yako haikumbuki ulichokuwa unakinena basi hayo ni machafuko na ni kazi ya roho mchafu, 3. Lugha wanayoinena iwe inaeleweka kwa wasikilizaji: 1 Wakorintho 14:9 "Vivyo hivyo na ninyi, msipotoa kwa ulimi neno lililo dhahiri, neno lile linenwalo litajulikanaje? Maana mtakuwa mkinena hewani tu." Je, ni kweli lugha zinazo nenwa siku hizi makanisani zipo dhahili kwa watu au (wanazielewa)? 4. Lugha isipoeleweka huo ni ujinga. 1 Wakorintho 14:11 "Basi nisipoijua maana ya ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye; naye anenaye atakuwa mjinga kwangu." Mfano: Unafika mahali unaanza kunena kwa Kingereza wakati hakuna hata mtu mmoja kati yao anayejua Kingereza:, wewe unenaye utakuwa mjinga, na wewe utawaona wale unaowanenea ni wajinga maana hawaitikii kile unachokinena. 5. Ikiwa mtu anataka kunena kwa lugha basi awepo mtu wa kutafsiri hiyo Lugha. 1 Wakorintho 14:13 " Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri." Na kama hakuna mtu wa kutafsiri hiyo lugha basi asinene, maana hakuna atakayemuelewa anachonena: 1 Wakorintho 14:28 "Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu." Je, ni kweli mnaponena kwa lugha kuna mtu wa kutafsiri au kila mtu ananena apendavyo? Ndani ya Kanisa watu wa kunena wawe wawili au watatu tu. Zaidi ya hapo ni machafuko. 1 Wakorintho 14:27 "Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri." Je, ni kweli makanisani siku hizi wananena wawili au watatu? Haitakiwi Kanisa zima linene kwa Lugha, maana yatakuwa ni machafuko. 1 Wakorintho 14:23 "Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu?" Kunena kwa Lugha ni karama inayotolewa na Roho Mtakatifu kwa mtu ampendaye, na sio kwa kila mtu ndani ya kanisa ni lazima anene kwa lugha, na hivyo kulazimisha watu wanene kwa lugha au kuwafundisha watu jinsi ya kunena kwa lugha ni makosa makubwa, maana Roho Mtakatifu ndiye anayemfundisha mtu jinsi ya kunena na sio mwanadamu; 1 Wakorintho 12:28-30 "Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha. Je! Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri?" NOTE: Ikiwa kanisani haiwezekani watu wote wakawa Manabii au waalimu au waponyaji, inakuwaje leo makanisani mlazimishe kila mtu anene kwa lugha? Kunena kwa lugha ni moja ya Karama kama zilivyo karama nyingine. 1 Wakorintho 12:4, 7-11 "Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule….Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye." Kwa hiyo ukiona mtu haneni kwa Lugha ujue Mungu amempa karama nyingine kati ya hizo, inawezekana amepewa karama ya Hekima au Maarifa au Karama ya kuponya NK. LUGHA YA MALAIKA Hakuna mwanadamu aliye wahi kuongea lugha ya malaika katika Biblia; bali Biblia inawaonyesha malaika wakiongea na Wanadamu kwa lugha ya binadamu yenye kueleweka kwa wanadamu waliopelekewa ujumbe. Mfano: Mwanzo 19:15-22 Malaika wale wawili waliongea na Lutu juu Sodoma na Gomora kwa lugha ya Wanadamu ya kueleweka. Danieli 9:21-27. Malaika Gabrieli aliongea na Danieli lugha ya kibinadamu ya kueleweka kwa Danieli. Mifano ni mingi.!! HITIMISHO: Ukweli ni kwamba utaratibu wa kunena kwa Lugha unaofanyika katika makanisa mengi yanayojiita ya kiroho ni kinyume kabisa na Biblia, mfumo huo ni wakipagani: Hakuna utofauti na waganga wa Kienyeji. Mganga wa kienyeji ili aiite mizimu yake ni lazima asisimuliwe kwa ngoma na matunguli, kisha huanza kunena kwa lugha za mizimu yake ili ishuke, Ndivyo ilivyo Makanisani siku hizi ili roho mchafu ashuke ni lazima watu wasisimuliwe kwanza na nyimbo na ngoma, kisha huanza kunena kwa lugha zisizojulikana. BWANA ATAWARUDISHIA WAKOMBELEWA LUGHA SAFI. Sefania 3:8-9 "...dunia yote itateketezwa kwa moto wa wivu wangu. Maana hapo ndipo nitakapowarudishia mataifa lugha iliyo safi, wapate kuliintia jina la Bwana, wamtumikie kwa nia moja." NOTE: Mtu akipagawa na mapepo mara nyingi huangushwa chini na kugaagaa huku akipiga kelele, pasipo yeye mwenyewe kujielewa, Na wanaodai hujazwa na Roho Mtakatifu kwa kunena kwa Lugha vivyo hivyo wengi wao huangushwa chini na kuanza kupiga kelele na kugaagaa chini, pasipo wao wenyewe kujielewa.. Je, utamtofautisha vipi mtu mwenye mapepo na mwenye Roho? Bila shaka wote ni kundi moja hakuna utofauti. NB: Haijawahi kutokea ndani ya Biblia Mtu aliye jazwa na Roho Mtakatifu akaangushwa chini, bali waliopagawa na mapepo tu ndio huangushwa chini. Mtu aliyejazwa na Roho Mtakatifu hatambuliwi kwa kunena lugha zisizojulikana, Bali hutambuliwa kwa tunda la Roho Wagalatia 5:22-23 "Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria." Sasa mtu aliyejazwa na Roho Mtakatifu ajipime hapo,na sio kunena kwa Lugha zisizojulikana, maana wapo watu wananena kwa lugha lakini bado matendo yao ni ya mwilini Wagalatia 5:19-21 "Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu" BWANA AKUBARIKI SANA. MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 16:21, 2 January 2021 (UTC)[reply]

JE, WAFU WATAFUFULIWA???

[edit]

U F U F U O. Faraja ya waliokufa katika Yesu Kristo.

"Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo." (Yohana 11:25)

"Wafu wako watafufuka, maiti zangu zitafufuka, amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini..."(Isaya 26:19)

"Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamuka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele." (Daniel 12:2)

"Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, na mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake." (Ufunuo 20:13)

Mwanadamu, aliyeumbwa kutoka mavumbini, hurudi mavumbini wakati wa kufa.

Mungu akamwambia Adamu:

"...hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi." (Mwanzo 3:19)

Mwanadamu akifa hulala katika mavumbi ya ardhi. Ikiwa kama alikufa katika Bwana, atangojea mpaka atakapofufuliwa tena wakati wa kurudi Kwa Yesu Kristo mara ya pili.

NI NINI KILISABISHA KIFO?

"Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi. (Warumi 5:12)

"Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23)

"Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti..." (Warumi 6:23)

ATAKAYEWAFUFUA WALIOKUFA NI NANI?

"Amin, amin, nawaambia, saa inakuja, na saa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai. (Yohana 5:25)

"Na mapenzi yake aliye nipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho." (Yohana 6:39)

"...ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na Uzima wa milele; Nami nitamfufua siku ya mwisho." (Yohana 6:40)

"Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo" (Yohana 11:25)

Yesu ndiye atakaye wafufua wafu wote.

NI NANI ALIYE NA FUNGUO ZA MAUTI NA KUZIMU (MAKABURI)

"... na aliyehai, nami nilikuwa nimekufa na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti na kuzimu." (Ufunuo 1:18) Yesu Ana funguo za mauti.

UFUFUO UTAKUWA KTK MAKUNDI MANGAPI?

"Msisitajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu." (Yohana 5:28,29)

"Nina tumaini kwa Mungu... ya kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, wenye haki na wasio haki pia." (Matendo 24:15)

1.Kuna ufufuo wa wenye haki unaitwa pia ufufuo wa uzima,

2.Na Kuna ufufuo wa wasio haki unaitwa pia ufufuo wa hukumu.

UFUNUO WA KWANZA.

UFUFUO WA KWANZA UTAKUWA LINI?

"Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza." (1 Wathesalonike 4:16)

WATAKATIFU WATAFUFULIWA KATIKA UFUFUO WA NGAPI?

"Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri na mtakatifu ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu." (Ufunuo 20:6)

Ufufuo wa kwanza unaitwaje?

"...Kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki" (Luka 14:14) "Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima." (Yohana 5:29)

Ufufuo wa kwanza unaitwa ufufuo wa uzima, pia unaitwa ufufuo wa wenye haki.

Watakaokutwa wamempokea Yesu, wakiwa hai, siku ya kuja Yesu, nini kitawapata?

"Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani, hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele..."(1 Wathesalonike 4:17)

"Angalieni nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika." (1Wakorintho 15:51-53)

Mungu atawaamsha wafu, akiwapa tena pumzi ya uhai, na kuiamuru mifupa ipate kuishi.

"Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka, amkeni kaimbeni ninyi mnaokaa mavumbini..." (Isaya 26:19)

Paulo anaeleza kwamba wenye haki; "Watamlaki Bwana hewani" hawatabakia katika dunia hii. (1Wathesalonike 4:17)

Yesu alisema: "...Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu. (Yohana 14:3,4)

Baada ya watakatifu kufufuka, nini kitatokea?

"Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pande nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu." (Mathayo 24: 31)

UFUFUO WA PILI (WA WENYE DHAMBI) UTAKUWA LINI?

"Hao wafu waliosalia hawakuwa hai hata itimie ile miaka elfu." (Ufunuo 20:5)

Kwa kuwa waovu hawataweza kwenda mbinguni kwa sababu hawakumpokea Yesu kama mwokozi wao, hawana sababu ya kufufuka Yesu atakaporudi duniani. Watabakia katika makaburi yao mpaka miaka elfu imalizike. Ndipo watafufuliwa ili wapate hukumu yao.

Mwishoni mwa miaka elfu, waovu watafufuliwa Kwa kusudi gani?

"Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake." (Mathayo 25:41)

"Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa katika lile ziwa la moto." (Ufunuo 20:15) Watu wa namna gani watakaochomwa moto wa milele?

"Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, Sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. (Ufunuo 21: 8)

Je! Baada ya kuchomwa moto, watenda dhambi watakumbukwa tena?

"Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika siku ile niifanyayo, asema BWANA wa majeshi." (Malaki 4:3)

"...nao watakuwa kama kwamba hawakuwa kamwe." (Obadia 16)

"Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo." (Zaburi 37:10)

W I T O:

Mwamini Bwana Yesu, ili akufufuwe katika ufufuo wa zima, siku ya mwisho.

"...kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho" (Yohana 6:40) MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 06:31, 29 January 2021 (UTC)[reply]

JE! KATI YA ROHO MTAKATIFU NA SHETANI; NI NANI ANAYEPINGA AMRI ZA MUNGU?

[edit]

BIBLIA INAJIBU

"Mkinipenda MTAZISHIKA AMRI zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa MSAIDIZI mwingine, ili akae nanyi hata milele. Ndiye ROHO wa kweli, ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea,..." (Yohana 14:15-17)

ROHO mtakatifu ☝anakaa ndani ya washika amri za Mungu.

Roho mtakatifu hapingi amri za Mungu.

Yohana 14:15-17 inaonyesha kuwa wanaompenda YESU watashika amri zake, naye Mungu atawapa msaidizi, yaani Roho mtakatifu. Kinyume chake ni: ukikataa amri za Mungu, huna Roho mtakatifu.

"Nami nitawapa moyo mmoja, NAMI NITATIA ROHO MPYA NDANI YAO, nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao. ILI WAENDE KATIKA AMRI ZANGU na kuyashika maagizo yangu , na kuyatenda; nao watakuwa Watu wangu, Nami nitakuwa Mungu wao"

             (Ezekiel 11:19,20)
Roho mtakatifu ☝  huwaongoza watu wake Mungu kushika amri za zake.

"Nami nitatia ROHO yangu ndani yenu na kuwaendesha katika SHERIA zangu..." (Ezekiel 36:27)

Huelewi hata hili☝ andiko kweli?

Roho mtakatifu huwaendesha watu wa Mungu washike sheria zake.

Roho mtakatifu anapoingia Moyoni mwa mtu ambaye moyo wa jiwe umeondolewa, ndipo mtu anaweza kushika amri za Mungu.

"...Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake" (Warumi 8: 9) "Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu." (Yohana 3:5)

☝Roho mtakatifu ndiye anayetuendesha na kutupatia uwezo wa kushika amri na sheria za Mungu.

"Ili maagizo ya Torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda Kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho." (Warumi 8:4)

Wanaoenenda☝ kwa kufuata Mambo ya Roho mtakatifu watayatimiza maagizo ya Torati (Sheria za Mungu)

Je! Watu waliokuwa na Roho mtakatifu walishika pia Amri za Mungu.?

DAUDI ALISHIKA AMRI ZA MUNGU NA ALIKUWA NA ROHO MTAKATIFU.

Daudi alikuwa na👇 Roho mtakatifu.

"Usinitenge na uso wako, wala Roho yako mtakatifu usiniondolee." ( Zaburi 51:11)

Daudi pia alishika👇 amri za Mungu.

"...walakini wewe hukuwa kama mtumishi wangu Daudi, ALIYEZISHIKA AMRI ZANGU na kunifuata kwa moyo wake wote,..."

  (1Wafalme 14:8)
Roho mtakatifu huwaongoza watu kushika amri za Mungu.

JE! YESU ALIKUWA NA ROHO MTAKATIFU? 👇

"Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akaenda Galilaya..." (Luka 4:14)

Yesu akasema: "Roho wa Bwana yu juu yangu,..." (Luka 4:18)

ROHO MTAKATIFU ALIMWONGOZA YESU KUSHIKA👇 AMRI ZA MUNGU.

"Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, Kama vile Mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake."

  (Yohana 15: 10)

Yesu alikuwa na Roho mtakatifu (Luka 4:18); Lakini pia alishika amri za Mungu. (Yohana 15:10)

Roho mtakatifu hata siku moja hatawaonzoza watu kupinga amri za Mungu.

NANI ANAWAONGOZA WATU KUZIKATAA👇 AMRI NA MUNGU?

"Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari." (Ufunuo 12:17)

Joka (Shetani) ana vita☝ ya kupinga watu wasishike amri za Mungu.

NIA YA MWILI INAPINGA AMRI ZA MUNGU, NIA YA ROHO HAIPINGI AMRI ZA MUNGU.

"Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kutii."

    (Warumi 8:7)

UKIFUATA MAMBO YA ROHO UTATII TORATI YAANI👇 SHERIA YA MUNGU.

"Ili maagizo ya Torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho." (Warumi 8:4)

"Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi..." (Yakobo 4:7,8)

TII AMRI NA MAAGIZO YA MUNGU UPEWE ROHO MTAKATIFU. "Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio." (Matendo 5:32)

Ubarikiwe sana msomaji wangu. MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 16:46, 8 February 2022 (UTC)[reply]

Waafrika katika biblia

[edit]

Tunaweza kusema kwa kiwango cha uhakika ya kwamba, ndiyo, Biblia inataja watu weusi, ingawa Biblia haitambui wazi mtu yeyote kuwa mwenye ngozi nyeusi. Pia, Biblia haitambui mtu yeyote kama mwenye ngozi nyeupe. Rangi ya ngozi ya mtu haijatajwa sana katika Biblia; rangi ya ngozi ya mtu haina maana kwa ujumbe wa msingi wa Biblia.

Hadithi nyingi za Biblia zinafanyika katika Mashariki ya Kati, ndani na karibu na Israeli. Watu "weusi" na "weupe" sio wengi katika mikoa hii. Watu wengi katika Biblia ni wa Kisemiti na wangekuwa rangi ya maji ya kunde. Hatimaye, haijalishi rangi ya ngozi watu wa Biblia walikuwa na nayo.

Wasomi wengine wanadhani kwamba mke wa Musa, Zippora, alikuwa mweusi kwa sababu alikuwa Mkushi (Hesabu 12: 1). Kushi ni jina la kale la eneo la Afrika. Shulammite inawezakana alikuwa mweusi (Wimbo Ulio bora wa Sulemani 1: 5), ingawa muktahdha unaonyesha kwamba ngozi yake ilikuwa nyeusi kutokana na kufanya kazi kwenye jua. Wengine hupendekeza kwamba Bathsheba (2 Samweli 11: 3) alikuwa mwenye ngozi nyeusi. Wengine wanaamini kwamba Malkia wa Sheba aliyemtembelea Sulemani (1 Wafalme 10: 1) alikuwamwenye ngozi nyeusi. Simoni wa Kurene (Mathayo 27:32) inawezekana ali kuwa mwenye ngozi nyeusi, na pia "Simeoni aitwaye Nigeri" katika Matendo 13: 1. Mtumwa wa Ethiopia huko Matendo 8:37 alikuwa wa ngozi nyeusi. Waethiopia wanatajwa mara 40 katika Biblia, na tunaweza kudhani kwamba haya ni marejeleoo kwa watu weusi, kwa kuwa Waethiopia ni watu wa ngozi nyeusi. Nabii Yeremia aliuliza, "Je! Mtiopiya anaweza kubadili ngozi yake?" (Yeremia 13:23) — Dhana ya asili ni kwamba Yeremia anaelezea ngozi nyeusi.

Wengi wa walimu wa Biblia wanaamini kwamba watu wa rangi nyeusi ni wazao wa Nuhu, mwana wa Hamu (Mwanzo 10: 6-20), lakini hatuwezi kuwa na hakika kwa kuwa Biblia haswa haielezei, Biblia mara kwa mara iko kimya kwa mambo ya rangi ya ngozi. Rangi ya ngozi si muhimu kwa Mungu kama hali ya moyo. Injili ni habari njema ya ulimwengu wote. Watu wenye ngozi nyeusi, watu wenye ngozi nyeupe, na walio kati ya rangi hizi mbili wanaalikwa kuja kwa Kristo kwa ajili ya wokovu. Kwa neema ya Mungu tunaweza kuchukua macho yetu mbali na ngozi na kuzingatia roho.

Injili haiangalii ngozi injili ni hitaji la kila mtu


Tafadhali sambaza kwa wengine ambao wanadhani katika biblia hakuna watu weusi na wanadanganywa na shetani kuwa dini zimeletwa na wazungu ili kututawala. MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 10:17, 4 August 2024 (UTC)[reply]

BWANA WA SABATO MAANA YAKE NINI

[edit]

Bila shaka utakubaliana nami kwamba simu imetengenezwa kwa ajili ya mwanadamu, ina maana simu ni lazima imnufaishe na kumpa furaha huyu mwanadamu.

Kiatu kimetengenezwa kwa manufaa ya miguu ya mwanadamu, ina maana mwanadamu ina bidi anufaike au ajisikie furaha kwa kuvaa kiatu na ili mwili wake uwe salama.

Kiti kimetengenezwa kwa ajili ya mwanadamu, yaani inabidi mwanadamu ajisikie furaha na amani anapokaa kwenye kiti na wala kiti haipaswi kimpe majonzi mwanadamu.

Gari limetengenezwa kwa ajili ya mwanadamu, ina maana mwanadamu ni lazima ajisikie furaha kupanda gari au kuwa na gari.

Na Biblia inasema: Marko 2:27

Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa #ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato.

Yesu anasema sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, kuonesha kwamba mwanadamu ni wa thamani sana ameumbwa kwa mfano na kwa sura ya Mungu, na ndio maana Mungu akamzawadia mwanadamu pumziko la sabato ili asifanye kazi kama mtumwa. Na hivyo Yesu anabainisha sabato haipaswi iwe ni mzigo kwa mwanadamu kama ambavyo simu au gari bovu ni mzigo kwa mtumiaji, kama walivyofanya mafarisayo hata kukataza uponyaji siku ya sabato, bali sabato inabidi impe furaha mwanadamu kwa kupumzika kutoka katika pilipilika za kidunia, na kuuburudisha moyo mbele za Muumbaji wake, kwa kukumbuka matendo makuu ya Mungu ya Uumbaji.

Lakini zaidi kwamba Yesu anajitambulisha kwamba yeye ni Bwana au Muasisi au Mmiliki au ndiye aliyeiweka sabato.

#Marko 2:28

Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.

Yesu hasemi mimi ni sabato la hasha!! Bali anasema yeye ni Bwana wa sabato, kuonesha umiliki au mamlaka. Mfano nikisema mimi ni Bwana wa shamba hili. Je hapo ina maana gani? Je ina maana mimi ni shamba? La hasha!!! Bali inaonesha kwamba mimi ni mmili wa shamba hili.

Kwa hiyo kama unataka shamba basi onana na mimi. Na hivyo Yesu ndiye Bwana wa sabato, unapompokea Yesu anakutoa kwenye utumwa wa kiroho na kukupa pumziko la sabato kama zawadi na sio mzigo tena.

Yaani ni hivi sabato inakupa wewe fursa ya kupumzisha shughuli zote za kidunia na fikra zako zielekezwe kwa Muumbaji wako. Kwa hiyo Mungu sio Diktetor ni mwenye upendo na ndio maana ametoa siku ya sabato iwe ni pumziko kwa wakazi wote wa Dunia. Ikiwa shuleni, kazini tunapata muda wa kupumzika basi hata Mungu anakupenda na ndio maana kaiweka sabato.

Niwataki pumziko salama la Sabato kwa watu wote wa Mungu.

"Basi imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu" Waebrania 4:9. MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 10:21, 4 August 2024 (UTC)[reply]

Je, ni watu gani watakao ingia mbinguni

[edit]

ndugu yangu, watu wengi watakosa kuingia mbinguni hii ni kwa sababu shetani kawadanganya kuwa ""kila anaye hubiri jina la YESU au anaetoa mapepo au anaefanya miujiza mingi au kuimba nyimbo za injili basi ataingia mbinguni"" lakini biblia inatwambia hivi

👇👇

Mathayo 7:21-23

[21]Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

[22]Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

[23]Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

👆👆

*Lakini ni huzuni sana maana watu hao wanajuhudi sana kwenda kanisani, kutoa zaka na sadaka nk na mtume paulo anawasema hivi*

👇👇👇


*Rumi 10:1,2 "ndugu zangu nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu ni mwombayo MUNGU, ni kwaajili yao, ili waokolewe, kwa maana nawashuhudia kwamba WANAJUHUDI KWA AJILI YA MUNGU, LAKINI SI KATIKA MAARIFA"*

Je, maarifa hayo ni yapi?? 🤔🤔

👇👇

*hosea 4;6 (watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa mimi nami nitakukataa wewe usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa UMEISAHAU SHERIA YA MUNGU WAKO mimi nami nitawasahau watoto wako)*

Kumbeee 🤔🤔🤔 kumwamini YESU kunaambatana na utiifu wa amri za MUNGU na usipofanya ivo unaitwa *mwongo* maana imeandikwa


*1 yohana 2;3,4(na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye ikiwa tunashika AMRI ZAKE yeye asemaye nimemjua wala hashiki amri ni MWONGO wala kweli haimo ndani yake)*


Huzuni ni kuwa hata isaya 24;3-6 nae anasema watu tunajifanya tunampenda YESU kumbe hatujaacha wizi, uongo, mauaji nk na mbaya zaidi tumeibadili siku ya sabato toka jumamosi kwenda siku ya jumapili kama ndiyo sikukuu ya ibada katika juma. Kwa kweli ni huzuni sana


*SHETANI KADANGANYA TENA KUHUSU MIUJIZA JUU YA WANADAM ILI KUWAAMINISHA WATU KUWA KUKIWA NA MIUJIZA TU SEHEMU YOYOTE UJUE PANA MUNGU HAPO*


ukifikili kuwa miujiza ni uwepo wa MUNGU basi miujiza hii inayokuja na mingine inatendeka sasa lazima umwabudu shetani tuu


ufunuo 13:11-16 kisha nikaona mnyama mwingine akipanda juu kutoka katika nchi naye alikuwa na pembe mbili mfano wa wana kondoo AKANENA KAMA JOKA naye atumia uwezo wote wa Mnyama yule wa kwanza mbele yake naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama yule wa kwanza ambaye jeraha la mauti lilipona NAYE AFANYA ISHARA KUBWA HATA KUFANYA MOTO KUSHUKA TOKA MBINGUNI UJE MBELE YA WANADAM NAYE AWAKOSESHA WALE WAKAAO JUU YA NCHI KWA ISHARA ZILE ALIZO PEWA KUZIFANYA...................... AKIWAAMBIA WAKAAO JUU YA NCHI KUMFANYIA sanamu huyo mnyama................... AKAPEWA KUTIA PUMZI HATA SANAM YA MNYAMA INENE na kuwafanya hao wasio sujudu sanamu ya mnyama wauwawe naye awafanya wote .................. watiwe chapa ya mnyama mkono wao wa kuume au katika vipaji vya nyuso zao.


*kwa fungu hilo la ufunuo linatuonyesha kuwa shetani naye anatumia miujiza ili awadanganye watu wamkosee MUNGU sasa basi tusitazame miujiza ya mtu furani na tukasema ana MUNGU ndani yake kumbe anashetani ndani yake*


pia ufunuo 16;12-14 na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto mkubwa frati maji yake yakakauka........................... *NIKAONA roho TATU ZA UCHAFU ZILIZOFANANA NA VYULA ZIKITOKA KATIKA KINYWA CHA YULE JOKA NA KATIKA KINYWA CHA YULE MNYAMA NA KATIKA KINYWA CHA YULE NABII WA UWONGO HIZO NDIZO roho za mashetani ZIFANYAZO ISHARA ZITOKAZO NA KUWAENDEA WAFALME WA ULIMWENGU WOTE* KUWAKUSANYA KWA VITA YA SIKU ILE KUU YA MUNGU MWENYEZI"


*katika fungu hili hapa juu 👆 la ufunuo linatuonyesha wazi kua roho za mashetani zinawadanganya wengi kwa miujiza. Kwa hiyo ndugu tusitafute miujiza bali mtafute Yesu kristo pekee*


Mathayo 24:24

[24]Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, *nao watatoa ishara kubwa na maajabu;* wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.


Kwa fungu hilo 👆👆👆 YESU anatukumbusha kuwa manabii na mitume na makristo wengi wa uongo nao wanatumia miujiza kuwapoteza watu wa MUNGU. Kwa hiyo tusitafute miujiza bali tumtafute YESU katika kweli yake yaani biblia na maandiko mengine matakatifu


ndugu kumbuka pia hata musa alipo kuwa kwa farao wachawi wa farao waliweza kuiga miujiza ya musa kutoka 7;10-12. Hivyo sio kila muujiza ni muujiza toka kwa MUNGU


*lakini pia vipi kuhusu ROHO wa MUNGU?? Je kuna ROHO wa MUNGU na wa shetani??*


Ndiyo, kuna ROHO wa MUNGU na wa shetani. Tafadhali soma mafungu haya


1 Yohana 4:1

[1]Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.


Kwa fungu hili tunaambiwa tusiziamini kila ROHO bali tuzijalibu kama zimetoka kwa MUNGU au kwa shetani.


Ni vema pia tukakumbushana kuhusu hili

*2 kortho 11;12-15 (lakini nifanyalo nitalifanya ili niwapinge hao watafutao nafasi wasipate nafasi ili kwamba katika neno hilo wajisifiao waonekane kama sisi maana watu kama hao ni mitume wa uwongo watenda kazi kwa hila wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa kristo wala si ajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wawatumishi wa haki ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao"*

Kwa fungu hili tunakumbushwa kuwa watumishi wa shetani na shetani mwenyewe wamejigeuza wawekama watumishi wa MUNGU ili waweze kuwadanganya watu wa MUNGU.


Je, utawatambuaje watu hao???


*Isaya 8:20*

*[20]Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.*


Sharti watu hao lazima watii amri za MUNGU na wawe na imani ya YESU hivyo ndivyo hata ufunuo anasisitiza hilo 👇👇 kwa hiyo kwa matendo na maneno yao ukiyapia kwa imeandikwa basi utaona jinsi wanavyo pingana na neno la MUNGU.


*ufunuo 14:12( hapa ndipo penye subira ya watakatifu HAO WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU NA IMANI YA YESU)*


na pia shetani anapigana sana na hao wanao zishika amri za MUNGU NA KUWA NA USHUHUDA WA YESU ufunuo 12;17


Inasomeka hivi


*Ufunuo wa Yohana 12:17*

*[17]Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.*


*HITIMISHO*

Watakao enda mbinguni ni wale wotevambao wanatii amri kumi za MUNGU yaani hawaibi, hawazini, hawasemi uongo, hawavunji sabato (jumamosi), hawaui, hawaabudu miungu wengine na ikiwepo amri yoyote ile hawendi kinyume chake

Pia kwa habari ya imani ya YESU, wanamwamini kuwa ndiye anaewasafisha dhambi zile za kuzini, kuiba, kusema uongo, kuvunja sabato, kuua, kuabudu miungu wengine nk. pia ndiye mfalme wetu na BWANA wa MABWANA wetu. na ndiye njia ya uzima wetu.

Kama ufafanuzi mwingine zaidi gusa link hii


*https://youtu.be/NkL4aP_-GAI*

MUNGU akubariki sana unapo ikubali kweli yake MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 10:25, 4 August 2024 (UTC)[reply]

JE, NI NANI ALIEBADILI SIKU YA SABATO TOKA JUMAMOSI NA KWENDA JUMAPILI?

[edit]

🤔🤔🤔 watu wengi sana wanasema kwa kifo cha YESU pale msalabani na kufufuka kwake ndivyo vilivyo sababisha sabato itoke jumamosi na kwenda jumapili. Je, 🤔🤔 ni kweli jambo hilo??

*NB*

PANA SILI NZITO SANA KUHUSU SIKU YA SABATO JAPO WENGI KWA AKILI YA KAWAIDA YA KIBINADAM WANACHUKULIA KAWAIDA TU.

Ndugu tujifunze leo kuhusu kufa na kufufuka kwa yesu na ukweli kuhusu siku ya sabato lakini tutaanza kuifahamu historia ya sabato

.

.

.

.

Kwa kuwa kabla ya dhambi sabato ya siku ya saba ilikuwepo mwanzo 2:1-3. lakini baada ya dhambi MUNGU hakupenda mwanadam apotee bali apate uzima wa milele yohana 3:15-17. basi kabla hajaja aliweka vitu vingi ambavyo vilikuwa Vivuli vya ujio wa *YESU kristo*  mfano  wa vimvuli hivyo ni pamoja na

*1* patakatifu pa dunia ebrania 8,

*2* sabato ya kila tarehe 10 mwezi 7 walawi 23:26-32 walawi 16:29-31

*3* sabato ya mwaka wa saba walawi 25:1-7 kutoka 23:10-11 kutoka 21:2

*4* sabato ya miaka 49 walawi 25:8----

*5* mwandamo wa mwezi wa abibu kutoka 23:15 kutoka 34:18

*6* sikukuu za vinywaji walawi 28:18 kutoka 29:40,41 walawi 23:13

*7*  mikate isiyotiwa chachu mwezi wa 2 tarehe 14 siku saba torati 16:3 kutoka 13:6,7 kutoka 34:18

*8* kula sadaka ya unga walawi 2:10.  mambo mengine meeengi

.

.

.

Hayo yote 👆👆👆👆👆👆 yalikuwa kivuli cha ujio wa YESU KRISTO

.

.

🤔🤔🤔 kwani YESU alikuja kufanya nini hapa duniani?? 🤔🤔

YESU kristo alikuja duniani kumtafuta yule mdhambi alie asi pale edeni kwa kutotii.

.

Kwa hiyo basi mtume paulo katika wakolosai anatwaambia vitu hivyo vilikuwa ni vivuli vya ujio wa YESU ukisoma kolosai 2:16,17 na aliendelea kuwaambia kuwa tusiendelee kushika siku kama ya tarehe 14 mwezi wa 2 au ya tareh 10 mwezi wa 7 na miezi kama mwezi wa abibu, miaka ya sabato nk katika galatia 4:9-10 lakini baada ya vivuli kuondolewa kama kolosai 2:16,17 inavyo sema.  Biblia inatwambia imebaki (imesalia) sabato ya siku ya saba tu ambayo haikuwa kivuli kwani ilikuwepo hata kabla ya dhambi kuingia na ni kumbukumbu ya *uumbaji* Na hii iliwekwa kwa lengo la  *kwa matendo ya mwanadam yakili au yaonyeshe kuwa  MUNGU ndiye muumbaji* kwani unapofanya kazi siku sita na kupumzika siku ya sabato (jumamosi)  unapumzika (starehe) kama Mungu alivyopumzika(starehe) katika kazi zake baada ya uumbaji. *Ukifanya hivyo unakili wazi kabisa kwa matendo kuwa Mungu ndiye muumbaji.* Usipo fanya hivyo kwa vitendo unapinga kuwa Mungu sio muumbaji kwa hiyo vitu viliibuka tu. Na hilo ndilo lengo la shetani kuwa kwa matendo yetu tupinge kuwa Mungu sio muumbaji ila kwa maneno tukili kuwa ni muumbaji. Tukumbuke kuwa yakobo 2:17,26 """.......... Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake............... Maana kama vile mwili pasipo Roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa""""

.

Kwa hiyo usipopumzika siku ya saba [sabato] (jumamosi) imani ya kuamini MUNGU muumbaji inakufa.

*NB*

Mungu hapendi uvivu na anachukia uvivu mithali 6:6-11 kutoka 20:8-11 *HIVYO FANYA KAZI KWA BIDII SIKU SITA NA SIKU YA SABA PUMZIKA*

.

.

.

.

.

*WENGI WA WANADAM WA LEO WANASEMA TUNAPUMZIKA JUMAPILI KWANI KWA KIFO NA UFUFUO WA YESU ULIHAMISHA UTUKUFU WA SIKU YA SABA (JUMAMOSI) NA KUIPELEKA JUMAPILI (SIKU YA KWANZA YA JUMA)*

🤔🤔🤔 je, jambo hilo ni kweli??? 👆👆👆

.

.

.

Kwa kuwa *"kwa mtu mmoja alipoasi wanadam wote wakaingizwa dhambini lakini kwa kutii kwa mtu mmoja wanadam wote wamepata haki Warumi 5:19"* kwa hiyo kwa kupigwa (kufa) kwa kristo pale msalabani wanadam wote tuliponya katika dhambi 1 petro 2:24 au wanadam wote tulinunuliwa kuwa wana wa MUNGU kupitia damu yake KRISTO ufunuo 5:9.

*hivyo siku ya UKOMBOZI wa mwanadam ni siku ya ijumaa* ambayo ndiyo siku kwa msalaba  wake akatufanya kuwa wa moja na haki sawa kwa wanadam wote katika kumwendea MUNGU

Waefeso 2:12-13,16

[12]kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.

[13]Lakini sasa, katika Kristo Yesu, *ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo.*

[16]Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba.

Ujanja wa mtu yoyote ni msalaba au kifo cha kristo YESU na sio vitu vingine 1 koritho 1:18

Lakini baada ya kufanya kazi ya UKOMBOZI, YESU alipumzika (starehe kaburini), kwani kwa kauli za YESU na MBINGU, kifo kinaitwa usingizi

👇👇

Yohana 11:11,13-14

[11]Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, *Rafiki yetu, Lazaro, amelala;* lakini ninakwenda nipate kumwamsha.

[13]Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala usingizi.

[14]Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, *Lazaro amekufa.*

👆👆

Kama Tunavyo faham, mtu baada ya kufanya kazi, anapumzika vivyo hivyo baada ya YESU kutukuomboa *(KUMUUMBA MWANADAM UPYA)* alipumzika sio kwamba alichoka bali ni kudhihilisha kuwa MUNGU ANAFANYA VITU KIKAMIKIFU NA VYEMA (kwa upendo MUNGU anamuumba mwanadam upya kama alivyo muumba mwanzo katika edeni kwa njia ya msalaba)

*NB*

MUNGU alipomuumba mwanadam alifanya kila kitu kiusahihi na baada ya kuanguka mwanadam dhambini akamuumba tena kwa mala ya pili siku ile ile ya *sita* kisha akapumzika au akalala siku ya saba *(hii yote ni kuonyesha kuwa alichokiumba mwanzo kilikuwa chema na hakina kasolo HIVYO ALIULUDIA ULE ULE UUMBAJI KWA MWANADAM ALIE KENGEUKA KATIKA ULE ULE UKAMILIFU WA MWANZO WA UUMBAJI)*

*usingizi ni PUMZIKO* kwani wengi wakichoka hua wanathubutu kuwaambia watoto wao kuwa *mtu akija mwambia baba hayupo, mi nalala sitaki mtu aje anisumbue*

LAKINI KWA KRISTO SIO KWAMBA ALICHOKA BAADA YA KUFANYA KAZI YA UKOMBOZI, Bali ilikuwa ni kumkumbusha mwanadam kuwa siku ya sabato ni zawadi kwake na siku hiyo ni alama au ni ishara kati ya MUNGU na mwanadam kwani mwanadam kwa matendo anakili kuwa MUNGU ndiye MUUMBAJI WAKE.

*HIVYO YESU KUWA KABURINI SIKU YA SABATO BASI ALIPUMZIKA AU ALIITUNZA PIA SABATO*

SIKU YA UFUFUO (SIKU YA KWANZA YA JUMA)

🤔🤔🤔 *kwanini YESU alifufuliwa siku ya kwanza ya juma* ??? 🤔🤔

*1* kwa sababu mauti haikustahili iendelee kumshikilia kwani kazi iliyomleta ya hapa duniani ni kumkomboa mwanadam kutoka dhambini na UKOMBOZI ulifanyika ijumaa

Matendo ya Mitume 2:24

[24]ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.

Waebrania 4:15

[15]Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; *bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.*

YESU hakuwa na dhambi hivyo mauti haikustahili imshikilie

👇👇

Warumi 6:23

[23]Kwa maana *mshahara wa dhambi ni mauti;* bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

*2* kumpatia tumaini mwanadam kuwa atafufuliwa

2 Wakorintho 4:14

[14]tukijua ya kwamba yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi nasi pamoja na Yesu, na kutuhudhurisha pamoja nanyi.

*3* akafanye huduma ya maombezi hekaru la mbinguni waebrania 8:1-7

*4* akaipeleke sadaka iliyotolewa pale msakabani

Ufunuo 5

*hivyo YESU KRISTO tangu alipofufuliwa na kweli akafufuka tunasema ameshinda mauti kwani tangu alipofufuliwa hadi leo na kesho hata milele na milele yu hai.*

HIVYO hakuna sababu yoyote ya kufanya ibada siku ya kwanza ya juma (jumapili) kama ndiyo sikukuu ya wiki katika ibada

*Hivyo ndugu zangu tuikumbuke siku ya sabato (jumamosi) na tuitakase*

.

.

Isaya 1:19-20

[19]Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;

[20]bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya

Lakini kwa mapana zaidi kuhusu ni nani alieibadili siku ya sabato gusa link hii

👇👇

https://youtu.be/x9RrQwheMdw

👆👆.

Ubarikiweeee *sambaza kwa wengine tafadhali* 🙏🙏🙏🙏🙏 MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 10:27, 4 August 2024 (UTC)[reply]

je, wasabato ni kina nani

[edit]

WASABATO NI KINA NANI?

Je, ni wakristo au wayahudi

Nimeona vyema leo tuchambue kwa ndani juu ya watu wanaoitwa wasabato.

Wasabato ni watu ambao wanaheshimu na kuadhimisha siku ya sabato, jina lao linatokana na msisitozo wanaouweka kwenye kuiheshimu siku ya sabato. Pengine utauliza siku ya sabato ndo siku gani? Mbona katika lugha ya kishwahili hamna siku inaitwa sabato?

           Neno sabato ni neno la Kiswahili lililotoolewa kutoka katika lugha ya kiebrania . katika lugha ya kiebrania neno hili linasomeka Shabbat lenye maana ya pumziko. Katika lugha ya kiebrania kuna siku inaitwa Shabbat, ambayo siku hiyo kwa Kiswahili inaitwa jumamosi.

. .

Angalia majina ya siku katika kiebrania na kiingereza,

English Name Hebrew "Name" Hebrew Meaning kiingereza kiebraniia maana ya kiebrania Sunday---- Yom Reeshone First day Monday -----Yom Shaynee Second day Tuesday------ Yom Shlee´shee Third day Wednesday ------Yom Revee´ee Fourth day Thursday ------- Yom Khah´mee´shee Fifth day Friday ------- Yom Ha´shee´shee Sixth day Saturday ------- Shabbat Rest . .

Kutoka kwenye neno Shabbat (sabato) , wote wanaoiheshimu na kuitunza siku ya sabato(jumamosi/Shabbat) wanaitwa wasabato. Wasabato hawa wamegawanyika katika makundi tofauti kama ifuatavyo. . .

1. JUDAISM / WASABATO WA DINI YA KIYAHUDI Hawa ni wasabato ambao historia yao ni ya kale sana . wanapatikana sana katika nchi ya Israeli , dini yao chimbuko lake ni katika biblia hasa agano la kale, Pamoja kwamba wasabato hawa wanaiheshimu siku ya sabato, jambo linalowatofautisha na wasabato wengine, ni kule kuamini kwao kuwa Yesu siyo masihi .

                    Wasabato hawa wa dini hii ya kiyahudi hawaamini kuwa Yesu ndiye kristo/masihi. Wanakubali kuwa Yesu alikuwepo ila hawakubali kuwa Yesu ndiye masihi aliyetabiriwa kwenye biblia agano la kale. Wao bado wanangojea ujio wa masihi atakayezaliwa ambaye atazaliwa Israeli na kuliongoza taifa hilo kuwa taifa lenye kuheshimika dunia kote.
                   Wasabato hawa wa dini ya kiyahudi wanashikilia msimamo wa babu zao ambao ndio walikuwa wapinzani wakubwa wa Yesu. Unaposoma katika biblia agano jipya utakutana na watu wanaitwa waandishi, makuhani na mafarisayo ambao walikuwa wakimpinga sana Yesu. Imani ya watu hawa haikupotea ila waliendelea na Imani hii na sehemu kubwa ya wanachi wa Israeli waliendelea kuwa waumini wa dini hii. Hata muisraeli asiyekuwa na Imani yoyote ujikuta akijumishwa katika Imani hii. Taifa la Israeli linasisitiza sana uadhimishaji wa sabato sheria za nchi zinazuia kufanya shughuli kazi siku ya sabato, na mwezi wa kwanza 2018 bunge la taifa hilo lilipitisha sheria ya kuzuia biashara siku ya sabato (jumamosi).

. . . . . .

2.WAKRISTO WASABATO/ KANISA LA KRISTO LA AWALI Kundi lingine la wasabato ni lile la wakristo wa awali, Kundi hili lilizaliwa kutoka katika dini ya kiebrania au dini ya kiyahudi, Mwanzilishi wa kundi hili ni Yesu. Wafuasi wa mwanzo kabisa walikuwa mwanzo waumini wa dini ya kiebrania (dini ya taifa la Israeli). Walikuwa wakisali pamoja na juadaism katika masinagogi na mahekalu siku ya sabato (jumamosi) luka 4:16, matendo 13:42-43. Kutokana na kuamini kuwa Yesu ndiye masihi/kristo, kundi hili liletengwa na masinagogi ya kiyahudi (yohana 16:2). Jamii kubwa ya waumini wa kundi hili mwanzoni walikuwa ni wayahudi baadae wakaongezeka na jamii ya mataifa mengine. Wasabato hawa waliendelea kuiheshimu na kuiadhimisha sabato ( matendo 16:13). Utanzaji wa sabato katika kundi hili ulikuwa tofauti na kundi lile lililo mkataa Yesu; wakati kundi lile lilizuia kuponya siku ya sabato (marko 3:2), kundi hili la wasabato-wakristo liliruhusu kuponya siku ya sabato, Wakati kundi lile lilisisitiza utoaji wa kafara siku ya sabato , kundi la wakristo- wasabato lilipinga utoaji wa kafara. Wakati kndi lile lilisisitiza tohara kama sehemu ya wokovu , kundi hili lilisisitiza tohara ya rohoni na ile ya mwili haikuwa na sehemu katika wokovu Makundi haya mawili yote yaliiheshimu sabato (jumamosi) lakini yalitofautiana namna ya kuiheshimu. . . . . . .

Kundi hili la wasabato wa kikristo liliendelea kuwepo kwa wingi hadi karne ya tatu( 300 AD), Ambapo katika kusanyiko la Laodikia (Council of Laodicea 363-364) ilipitishwa kwamba wakristo wasiendelee kupumzika siku ya sabato / jumamosi badala yake wapumzike jumapili.( waweza soma wikipedia na vyanzo vingene vya historia kuhusu council of laodicea na malengo yake makuu). . . .

Baada ya maamuzi haya waumini wengi wa kundi hili walihama na kuamua kuwa wajumapili (wanaopumzika siku ya jumapili) , Kundi hili la wasabato wakristo lilififia kiasi cha kuelekea kupotea kabisa maana yeyote aliyetaka kuendelea kuwa msabato alikabiliwa na mkono wa dola (selikali) ,mateso na kuuawa, ndipo wengi walijificha mapangoni na kuabudu kwa siri, kuendesha ibada za siku ya sabato ilikuwa kinyume na matakwa ya serikali ya Rumi. . . . . . . 3. SEVENTHDAY BAPTISTIST, Kundi hili la wasabato ni matokeo ya vuguvugu la matengenezo huko nchini Uingereza katika miaka ya 1650. Matokeo ya matengenezo yaliyoibuliwa na Martine Lutter mwanzilishi wa lutheran church katika miaka ya 1500 yalileta uamsho mkubwa wa watu kutaka kurudi katika misingi ya Biblia. Japo martine Luther mwenyewe hakupokea fundisho la ubatizo wa maji mengi, wanamatengenezo waliofuta walikuja na fundisho la ubatizo wa maji mengi, Fundisho hili lilipelekea kuzaliwa kwa dhehebu la Baptist church katika miaka ya 1520, Ndani ya hili dhehebu lilijitokeza kundi lingine ambalo liliamua kurudi kwenye sabato ya biblia ambalo ni SEVENTHDAY BAPTIST (SDB). Viongozi wake wa awali kina Mr Andreas Fischer na mke wake walihukumiwa kifo mwaka 1520 na baadaye kuuwa . wafuasi wa kundi hili walikuwa tayari kufa kuliko kuiacha sabato. Oswald Glait ni miongoni mwa wahubiri waloisambaza sabato maeneo ya ulaya , hata hivyo naye alikamatwa na kutupwa mtoni. Kundi hili la SDB lilitambulika kama dhehebu na kufanya mkutano wake wa kwanza uko uingereza mwaka 1651. Kundi hili la wasabato halikufanikiwa kukua sana, Kwa sasa lina waumini karibu 50, 000 wengi wa waumini hawa wapo maeneo ya India na marekani. Kutoka katika kundi hili la wasabato kulikuwa na muumini ,mama mmoja aliyeitwa Rechael Oaks ambaye aliileta sabato kwa kundi la waadventista na kupelekea kuzaliwa kwa wasabato tunaowafahamu waitwao sda. . . . . . . . . . 4.WAADVENTISTA WASABATO (sda) Kundi hili ndilo limeifufua sabato kwa kiasi kikubwa tangu ilipofifia enzi za mfalme constantine na kuitawanya sehemu kubwa ya dunia. Kundi hili lilizaliwa rasmi kama dhehebu la kikristo mwaka 1863 chini marekani. Waanzilishi wake karibu wote walikuwa ni wajumapili toka madhehebu tofauti kama babtist church, methodist church. Baadhi yao ni kina Joseph bates, James White, Ellen white na J N Andrews.

        Hawa wote walipokea fundisho la utunzaji wa sabato kutoka kwa mama mmoja iliyekuwa msabato aitwaye Rechael Oaks aliyekuwa muumini wa dhehebu la SEVENTHDAY BAPTIST . Waadiventista walilipokea fundisho la sabato na baadae fundisho kuhusu sabato lilidhibitishwa na maono ya Ellen G white , binti ambaye kipindi hiki alikuwa akipokea maono. Binti huyu alipewa maono na kuoneshwa amri za Mungu kumi la amri ya sabato ilionekana ikingaa sana. Kabla ya maono haya baadhi ya waadiventista walikuwa wameisha pokea fundisho la sabato na kulikubali na walikuwa tayari wameanza kupumzika na kufanya ibada siku ya sabato badala ya jumapili, E G White mwinyewe alikuwa amelipokea fundisho hili tayari.
                         Utunzaji wa sabato katika kundi hili unafanana kwa karibu sana na namna ulivyofanyika katika kanisa la kristo la awali. Kundi hili ufanya oponyaji siku ya sabato, pia kutembelea wagonjwa na waitaji siku ya sabato ni jambo linaloruhusiwa. Kundi hili linaitunza sabato katika kumtazama Yesu na wanafunzi wake walichokifanya siku ya sabato. Kama kuna shughuli yoyote ambayo Yesu aliifanya siku ya sabato basi shughuli hiyo ni halali kufanyika siku ya sabato katika kikundi hiki.

Kundi hili la wasabato ndo kundi pekee miongoni mwa makundi ya wasabato ambalo limefanikiwa kukua na kusambaa duniani karibu kila nchi japo zipo nchi ambazo halijawa na uongazi lakini waumini wapo. . .  Kwa ufupi nadhani umeelewa maana ya wasabato, na umefahamu makundi ya wasabato na tofauti zao. Somo hili liwasaidie wale wanaochanganya wasabato waliomkataa Yesu na wasabato wafuasi wa Yesu. .

(Marko 2: 27-28) Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia 196.249.105.27 (talk) 10:30, 4 August 2024 (UTC)[reply]

JE! WATU WA AGANO LA KALE NAO WALIOOKOLEWA KWA NEEMA ?

[edit]

FUNGU MAKUU: "Bwana asema hivi, Watu wale walioachwa na upanga walipata neema jangwani; yaani, Israeli, hapo nilipokwenda kumstarehesha."

 (Yeremia 31:2)

" Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;" (Tito 2:11)

Baadhi ya watu hudhani kuwa watu wa agano jipya tu ndio wanaokolewa kwa neema kwa njia ya imani, na watu wa agano la kale wao waliokolewa kwa kushika sheria. Mawazo hayo si sahihi kabisa na ni mawazo batili kabisa. Biblia inafundisha kuwa watu wote wanao okolewa na mauti ya milele wanaokolewa kwa neema kwa njia ya imani na si vinginevyo. Walioishi agano la kale na agano jipya, wote wanaokolewa kwa neema kwa njia ya imani kupitia Yesu Kristo.

"Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; " (Tito 2:11) Fungu hili linatangaza wazi kuwa ni neema ya Mungu tu ndiyo inayowaokoa watu wote.

Hakuna kitu kingine kinacho waokowa wanadamu tofauti na neema ya Mungu.

msisitizo wa fungu hili ni " neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote". Hivyo wanadamu wote wa agano la kale na agano jipya watakaoingia katika uzima wa milele wataokolewa kwa neema kwa njia ya kumwamini Yesu.

"Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.

 (Waefeso 2: 8,9)

Neema ni kupata kitu usichostahili. Wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Hatustahili tena kuishi milele, bali mauti ya milele ndiyo stahiki yetu, ila kwa neema ya Mungu, mauti iliyotukabiri ilifidiwa na Yesu kupitia kifo chake. "Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi." (Marko 10:45) "Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. (Warumi 5:8) "Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. ( Isaya 53:5)

Agano la kale nalo linasema Nuhu na Waisraeli waliokolewa kwa neema tu.

" Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana." (Mwanzo 6:8) "Bwana asema hivi, Watu wale walioachwa na upanga walipata neema jangwani; yaani, Israeli, hapo nilipokwenda kumstarehesha. "

 (Yeremia 31:2)

Kupitia neema waliyoipata Waisraeli jangwani; Biblia inataja idadi kubwa ya watu waliookolewa kupitia neema hiyo. Musa, Kalebu, Yoshua, Haruni, Finehasi ni baadhi yao. Neema ilitolewa lini? " Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia." ( Yohana 13:8)

Neema ilikuwapo tangu milele, kabla ya kuumbwa dunia, hivyo Adamu alipoumbwa, aliikuta neema ikisubiri uasi wake ili imwokoe. Neema ilifunuliwa kupitia kifo cha Yesu kristo msalabani. Kifo cha Yesu (Neema) kilipangwa kutokea kabla ya misingi ya dunia kuwekwa, kabla Adamu na Hawa hawajaumbwa na kuanguka dhambini. Watu wote waliikuta neema ikiwa tayari kuwaokoa. uchaguzi ulibaki kwao, kuipokea neema ili waokolewa au kuikataa ili kuangamia. Kafara na damu ya wanyama hazikuondoa dhambi za watu wa agano la kale. "Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. " (Waebrania 10:4) Kafara zote hizo hazikuchukua dhambi yoyote bali zilikuwa mbadala wa kafara halisi, yaani, Yesu Kristo: " Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! " ( Yohana 1:29 )

Neema ilikuja kupitia Yesu Kristo.

"Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo." (Yohana 1:17)

       Neema, Imani na sheria.

Biblia inasema wazi kuwa neema inayookoa lazima iwe na imani. "Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; " (Waefeso 2:8)

Hivyo bila neema yenye  imani hakuna wokovu japokuwa tayari tuna neema kupitia kifo cha Yesu.

Hakuna atakayempendaza Mungu asipokuwa na imani. "Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; ..." (Waebrania 11:6) Waisraeli waliopata neema jangwani

(Yeremia 31:2), walipokosa imani walifia jangwani, hawakuingia katika nchi ya ahadi.

,"Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao." (Waebrania 3:19)

Kazi ya neema.

Neema inatufundisha kukataa ubaya wa namna zote. " Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; " (Tito 2: 11,12) Hapo ndipo linapokuja swala la sheria na amri za Mungu. Sheria ya Mungu inafunua mabaya ambayo kwa mtu anayeokolewa kwa neema hapaswi kuyatenda. Dhambi ni matendo mabaya yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu ambayo yamefunulia katika amri kumi. Dhambi ni uvunjaji wa sheria. (1 Yohana 3:4) KJV. Hivyo kwa anayeokolewa kwa neema hawezi kuondelea kutenda dhambi, yaani kuvunja amri za Mungu. "Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? " (Warumi 6:1,2)

Neema , imani na sheria huenda pamoja.

Ndiyo maana Yesu mleta neema naye alishika amri za Mungu. "Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. "

 (Yohana 15:10). Yesu mleta neema anaagiza tushike amri zake. Anasema: "Mkinipenda, mtazishika amri zangu.   (Yohana 14:15)

Imani huthibitishwa kwa kushika sheria.

Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.     (Warumi 3:31)

Ndiyo maana Waisraeli waliookolewa kwa neema jangwani waliagizwa kushika amri za Mungu. Watu wa agano jipya nao wanaokolewa kwa neema, mitume na Yesu wanawahimiza kushika sheria na amri za Mungu. " Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. " (Yakobo 2:10,11) "Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu."

  "Ufunuo  14:12"

Watu wa agano la kale na agano jipya wanaokolewa kwa njia ileile moja, yaani neema, kwa njia ya imani, imani inayothibitishwa kwa kushika sheria. (Warumi 3:31) Fanya uamuzi sasa.

        Mungu akubariki sana.

Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu torati tazama somo hilo MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 10:36, 4 August 2024 (UTC)[reply]

JE! KATI YA ROHO MTAKATIFU NA SHETANI; NI NANI ANAYEPINGA AMRI ZA MUNGU?

[edit]

BIBLIA INAJIBU

"Mkinipenda MTAZISHIKA AMRI zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa MSAIDIZI mwingine, ili akae nanyi hata milele. Ndiye ROHO wa kweli, ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea,..." (Yohana 14:15-17)

ROHO mtakatifu ☝anakaa ndani ya washika amri za Mungu.

Roho mtakatifu hapingi amri za Mungu.

Yohana 14:15-17 inaonyesha kuwa wanaompenda YESU watashika amri zake, naye Mungu atawapa msaidizi, yaani Roho mtakatifu. Kinyume chake ni: ukikataa amri za Mungu, huna Roho mtakatifu.

"Nami nitawapa moyo mmoja, NAMI NITATIA ROHO MPYA NDANI YAO, nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao. ILI WAENDE KATIKA AMRI ZANGU na kuyashika maagizo yangu , na kuyatenda; nao watakuwa Watu wangu, Nami nitakuwa Mungu wao" (Ezekiel 11:19,20)

Roho mtakatifu ☝ huwaongoza watu wake Mungu kushika amri za zake.

"Nami nitatia ROHO yangu ndani yenu na kuwaendesha katika SHERIA zangu..." (Ezekiel 36:27)

Huelewi hata hili☝ andiko kweli?

Roho mtakatifu huwaendesha watu wa Mungu washike sheria zake.

Roho mtakatifu anapoingia Moyoni mwa mtu ambaye moyo wa jiwe umeondolewa, ndipo mtu anaweza kushika amri za Mungu.

"...Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake" (Warumi 8: 9) "Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu." (Yohana 3:5)

☝Roho mtakatifu ndiye anayetuendesha na kutupatia uwezo wa kushika amri na sheria za Mungu.

"Ili maagizo ya Torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda Kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho." (Warumi 8:4)

Wanaoenenda☝ kwa kufuata Mambo ya Roho mtakatifu watayatimiza maagizo ya Torati (Sheria za Mungu)

Je! Watu waliokuwa na Roho mtakatifu walishika pia Amri za Mungu.?

DAUDI ALISHIKA AMRI ZA MUNGU NA ALIKUWA NA ROHO MTAKATIFU.

Daudi alikuwa na👇 Roho mtakatifu.

"Usinitenge na uso wako, wala Roho yako mtakatifu usiniondolee." ( Zaburi 51:11)

Daudi pia alishika👇 amri za Mungu.

"...walakini wewe hukuwa kama mtumishi wangu Daudi, ALIYEZISHIKA AMRI ZANGU na kunifuata kwa moyo wake wote,..." (1Wafalme 14:8)

Roho mtakatifu huwaongoza watu kushika amri za Mungu.

JE! YESU ALIKUWA NA ROHO MTAKATIFU? 👇

"Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akaenda Galilaya..." (Luka 4:14)

Yesu akasema: "Roho wa Bwana yu juu yangu,..." (Luka 4:18)

ROHO MTAKATIFU ALIMWONGOZA YESU KUSHIKA👇 AMRI ZA MUNGU.

"Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, Kama vile Mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake." (Yohana 15: 10) Yesu alikuwa na Roho mtakatifu (Luka 4:18); Lakini pia alishika amri za Mungu. (Yohana 15:10)

Roho mtakatifu hata siku moja hatawaonzoza watu kupinga amri za Mungu.

NANI ANAWAONGOZA WATU KUZIKATAA👇 AMRI NA MUNGU?

"Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari." (Ufunuo 12:17)

Joka (Shetani) ana vita☝ ya kupinga watu wasishike amri za Mungu.

NIA YA MWILI INAPINGA AMRI ZA MUNGU, NIA YA ROHO HAIPINGI AMRI ZA MUNGU.

"Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kutii." (Warumi 8:7)

UKIFUATA MAMBO YA ROHO UTATII TORATI YAANI👇 SHERIA YA MUNGU.

"Ili maagizo ya Torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho." (Warumi 8:4)

"Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi..." (Yakobo 4:7,8)

TII AMRI NA MAAGIZO YA MUNGU UPEWE ROHO MTAKATIFU. "Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio." (Matendo 5:32)

Ubarikiwe sana msomaji wangu.

Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu sheria au torati gusa link hii MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 10:37, 4 August 2024 (UTC)[reply]

JE, PETRO NI MWAMBA LILIPOJEGWA KANISA???

[edit]

KWA MUJIBU WA ANDIKO KUMHUSU PETRO

Mathayo 16 : 18 - Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

JE NI KWELI KWAMBA YESU KRISTO ALIMAANISHA KUJENGA KANISA JUU YA PETRO!!

JE, MADAI HAYO YAKO SAWA?

TUYAULIZE MAANDIKO AMBAYO NDIYO MSINGI WA UKRISTO WOTE.

TUANZE NA MAANA YA JINA LENYEWE YAANI #PETRO,

JINA HILI HALIKUWA LAKE TANGU KUZALIWA KWAKE, BALI ALIPEWA NA YESU SIKU WALIPOKUTANA KWA MARA YA KWANZA. 👇👇

Yohana 1 : 42 - Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).

JINA LAKE HALISI ALIITWA #SIMON YOHANA

YESU ANAMWITA

  1. KEFA YENYE MAANA MBILI, YAANI #PETRO AU #JIWE

LEO TUTASHUGHULIKA NA MAANA YA PILI YA JINA LAKE, YAANI #JIWE#

MBALI NA KUWA MWANAFUNZI WA YESU,

PETRO PIA NI MWANDISHI WA VITABU KATIKA BIBLIA.

VITABU ALIVYOANDIKA NI VIWILI, NAVYO NI:-

1. WARAKA WA KWANZA WA PETRO KWA WATU WOTE

2. WARAKA WA PILI WA PETRO KWA WATU WOTE.

TUMSIKIE SASA PETRO MWENYEWE ANASEMAJE JUU YA SUALA HILI,

1 Petro 2 : 5 - Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.

PETRO HAPA ANATWAMBIA KWAMBA SISI NASI NI #MAWE KAMA ALIVYO YEYE AMBAYE NI #JIWE.

WEWE NA MIMI NI MAWE TUNAOJENGA KANISA LA MUNGU.

PETRO ALIKUWA NI MTU WA KUSOMA MAANDIKO, TAZAMA ANANUKUU MANENO YA UNABII ULIOTOLEWA MIAKA MINGI ILIYOPITA KUPITIA NABII ISAYA 👇

Isaya 28 : 16 - kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.

LINGANISHA NA ALIVYOSEMA HAYO MANENO NA #1 Petro 2: 6 Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika. 1 Petro 2:6

🔐 1 Petro 2 : 7 - Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

PETRO ANAZIDI KUMTAMBULISHA #YESU KRISTO KUWA NDIYE #JIWE #KUU LA PEMBENI, LENYE HESHIMA.

HAISHII HAPO 👀👇🏽

1 Petro 2 : 8 - Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa neno lile,wasiliamini,nao waliwekwa kusudi wapate hayo.

BALI ANAMTAMBULISHA KUWA NI #MWAMBA

HIVYO PETRO NI JIWE LILILOJENGWA KATIKA #MWAMBA MKUU, #JIWE #KUU AMBAYE NI YESU KRISTO. WALE WANAOSEMA WAMEJENGA JUU YA PETRO WAKO SALAMA?

KOSA LIKO WAPI???

HEBU TULIANGALIE TENA FUNGU AMBALO WATU WAMEJENGA👇👇👇

Mathayo 16 : 18 - Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

KAMA TUNGEKUWA MUBASHARA AU LIVE WAKATI KAULI HII INATOLEWA NA YESU TUNGEONA NAMNA AMBAVYO ANAJIONESHEA KIDOLE YEYE MWENYEWE (YESU) KAMA #MWAMBA MKUU AMBAO #KANISA LINAJENGWA

YAANI:-

➡👤 WEWE NDIWE PETRO (JIWE)

NA

➡ JUU YA MWAMBA HUU👤👈🏽 (YESU KRISTO, #JIWE #KUU, #MWAMBA WA KALE) "NITALIJENGA KANISA LANGU"

ANGALIA 👇

1 Wakorintho 10 : 4 - wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.

JINA LA MWAMBA NI LA #YESU KRISTO MWENYEWE,

MWAMBA NI SIFA YA #MUNGU MWENYEENZI NA #KRISTO NI MUNGU ALIYEFANYIKA MWANADAMU KWA KUSUDI MAALUMU LA UKOMBOZI WA MWANADAMU.

PETRO KAMWE HANA SIFA YA KUWA MWAMBA, YEYE NI JIWE KAMA ILIVYO KWAKO NA KWANGU, SISI NI MAWE TINAOTAKIWA KUJENGA JUU YA MWAMBA YESU KRISTO.

Yohana 1 : 14 - Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu......... 🎁🎁🎁🎁🎁🎁🎁🎁🎁🎁🎁🎁 Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili. Kumbukumbu la Torati 32:4

Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake. Kumbukumbu la Torati 32:15

Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, Mungu aliyekuzaa umemsahau. Kumbukumbu la Torati 32:18

Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana asingaliwatoa? Kumbukumbu la Torati 32:30

Hakuna aliye mtakatifu kama Bwana; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu. 1 Samweli 2:2

Maana ni nani aliye Mungu, ila Bwana? Ni nani aliye mwamba, ila Mungu wetu? 2 Samweli 22:32

Wakakumbuka kuwa Mungu ni mwamba wao, Na Mungu Aliye juu ni mkombozi wao. Zaburi 78:35

Isaya 26 : 4 - Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.

♦♦♦♦♦♦♦♦♦♦♦♦♦♦♦♦♦♦♦♦

WITO! ➡JENGA JUU YA MWAMBA

➡ JENGA JUU YA YESU KRISTO ALIYE MWAMBA WA MILELE

Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; Mathayo 7:24 👇👇 MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 10:38, 4 August 2024 (UTC)[reply]

WAKOLOSAI SURA 2:16

[edit]

Bwana Asifiwe wana na binti za Mungu.

Mara nyingi nimekuwa nikiona watu wengi wakitumia fungu hili la Wakolosai 2:16, pasipo kujua maana yake halisi ni ipi?

Na hiki ndicho Petro anaonya juu ya nyaraka za Paulo:

2 #Petro 3:15-17 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa; vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.

Niseme tu kwamba nyaraka za Paulo zimepotoshwa sana na baadhi ya viongozi wa Dini, kwa kuwakaririsha waumini wao upotofu.

Sasa Aya yenyewe inasema:

  1. Wakolosai 2:16-18

Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.

Sasa watu wengi hupenda kunukuu hilo fungu, kama nyundo kwa dhehebu la SDA, katika kipengere cha Chakula na Sabato tu, mengine wana yaacha.

Hebu leo tugeuze kibao kidogo. 1. Je, mlevi anayetumia bia, akitumia fungu hili kwamba Usimuhukumu juu ya vinywaji, je atakuwa amekosea? 2. Je, Muislamu naye akikwambia usimuhukumu juu ya sikukuu ya mwandamo wa mwezi, kwa kutumia aya hiyo atakuwa amekosea? 3. Je, wanaokula binadamu wenzao, nyoka, mbwa nk. Wakitumia aya hii kwamba usiwahukumu, juu ya chakula, je watakuwa wamekosea?

Kwa hiyo kabla hujajenga hoja juu ya sabato, na ulaji wa nguruwe, fikiria kwanza endapo mlevi naye akakomaa na hilo fungu kwamba usimuhukumu juu ya vinywaji.

Hebu turudi kwenye pointi, Paulo wakati anaandika waraka huu kwa Wakolosai, tayari kulikuwa na walimu wa uwongo, walioingiza mafundisho potofu katika kanisa la Kolosai, Sasa ili uielewe maana halisi ya Wakolosai 2:16, ni vizuri kuanzia #aya ya 14: inasema:

  1. Wakolosai 2:14-15

akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.

Paulo anasema Yesu aliifuta #HATI iliyokuwa inatushitaki kwa #hukumu zake.

Kipindi cha Musa, kulikuwa na sheria za aina Mbili.

#AMRI kumi za Mungu, Amri 10, ziliandikwa na Mungu mwenywe kwa kidole chake katika mbao mbili za Mawe.
  1. Kumbukumbu la Torati 4:13

Akawahubiri agano lake, alilowaamuru kulitenda, yaani, zile amri kumi; akaziandika juu ya mbao mbili za mawe.

  1. Kutoka 31:18 Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu.

2) #SHERIA ZA MUSA, sheria hizi za Musa ziliandikwa na Musa yeye mwenyewe katika chuo,

  1. Kumbukumbu la Torati 31:9

Musa akaiandika torati hii, akawapa makuhani, wana wa Lawi, waliolichukua sanduku la agano la Bwana, na wazee wote wa Israeli.

Sasa katika torati ya Musa ndiko zilikoandikwa #Hukumu, na mambo yote yaliyokuwa ni Kivuli, kama jino kwa jino, Taraka, Tohara,Kupiga mawe wavunja sabato na wazinzi, Utaratibu wa ibada za kafara NK.

  1. Mfano wa hukumu ni
  1. Ø Katika Amri kumi za Mungu kuna amri, inasema #USIZINI inaishia hivyo tu, lakini ukienda kwenye torati ya Musa inasema, Mtu akikutwa anazini apigwe mawe hadi kufa. Kumbukumbu 22:22. Sasa kifo cha Yesu hakikuondoa Amri inayosema #USIZINI, bali kilichoondolewa ni hukumu ya kupiga mawe wazinzi.
  1. Ø Katika Amri kumi kuna amri: inasema #USIUE, inaishia hapo tu, lakini katika torati ya Musa inasema Mtu atakayeuwa naye Auawe, Kutoka 21:12, sasa kifo cha Yesu hakikuondoa amri ya USIUE, bali kilichoishia msalabani ni hukumu ya kuua muuaji.
  1. Ø Amri ya Mungu inasema Ikumbuke siku ya sabato uitakase, lakini Torati ya Musa inasema Mtu akivunja sabato lazima Auawe, sasa kifo cha Yesu hakikuondoa Amri ya kuitunza sabato, bali kilichoondolewa ni ile hukumu ya kupiga mawe mvunja sabato. Kutoka 35:1-3
  1. Ø Amri ya Mungu inasema USILITAJE BURE JINA LA BWANA MUNGU WAKO, lakini torati ya Musa inasema mtu akitaja jina la Mungu bure ni lazima Auwawe, sasa kifo cha Yesu hakikuondoa Amri inayosema USILITAJE JINA LA MUNGU BURE, bali kilichoishia msalabani ni Hukumu ya kifo kwa anaye litaja jina la Mungu bure/ kukufuru.

Na Paulo anabainisha kwamba kifo cha Yesu kiliondoa Hukumu na sio Amri.

  1. Wakolosai 2:14-15

akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;

Na ndio maana sasa hivi hata ukimkuta mtu anazini au anavunja sabato, hawezi akapigwa mawe kwa sababu ile hukumu ya kupiga mawe Yesu aliigongomelea msalabani.

  1. Warumi 8:1-2

Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

Torati ya Musa ndio ilikuwa inatoa Hukumu zote.

  1. Matendo ya Mitume 13:39

na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa.

Hivyo kilicho gongomelewa ni ile #HATI iliyoandikwa na Musa, ambamo mlikuwa na hukumu za kila aina.

Sasa kabla ya kujua Paulo alikuwa anamaanisha nini katika #Wakolosai 2:16, inabidi kutafakari kwanza aya ya 17,

  1. Wakolosai 2:17-18

mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.

Kwa hiyo inabidi ujiulize ni mambo gani hayo yalikuwa ni kivuli, yakilenga mwili wa Kristo? Tumeshaona pia zile Hukumu ndio zilikuwa zikilenga Kifo cha Yesu msalabani. Wakati Yesu alipokufa pale msalabani Pazia la Hekalu lilipasuka vipande viwili, hii iliashiria kwamba huduma zote zilizokuwa zikifanyika Hekaluni zilikuwa kivuli, zikielekeza kifo cha Yesu,

  1. Mathayo 27:50-52

Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi . Na Paulo anathibitisha kwamba huduma za patakatifu/ Hekalu zilikuwa ni kivuli.

  1. Waebrania 8:5 watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.

Sasa mambo yote ambayo Paulo ameyaorodhesha katika #Wakolosai 2:16 yalikuwa yakifanyika Hekaluni, ikiwa na maana zaidi kwamba yalikuwa yakiambatana na utoaji wa kafara zilizofanyika Patakatifu/ Hekaluni. Na kafara zote zilikuwa zinamlenga Yesu.

#VYAKULA.

· Kulikuwa na mikate ya wonyesho, iliyokuwa inaliwa na Makuhani. Mambo ya walawi 24:5-9 · Malimbuko yote kilikuwa chakula cha makuhani. Kumbu 18:1-5 2. #VINYWAJI; · Kulikuwa na malimbuko ya vinywaji, yaliyoambatana na utoaji wa kafara Kutoka 22:29-30 Usikawie kuleta malimbuko ya matunda yako na ya vinywaji vyako. Na Divai iliyokuwa inatolewa malimbuko, ilikuwa ni Kinywaji cha Makuhani, Kumbu 18:4

3. #SIKUKUU. · Kulikuwa na sikukuu nyingi zilizoambatana na utoaji wa kafara ndani ya Patakatifu/ Hekalu.; kama sikuu ya Mavuno, sikukuu ya upatanisho, sikuu ya malimbuko NK. Soma Mambo ya walawi sura ya 23. Sherehe zote ziliambatana na utoaji wa kafara, ambazo ni kivuli cha Yesu.

4. #MWANDAMO WA MWEZI: · Kila mwezi ulipoandama kulikuwa na sikukuu, pia iliambatana na utoaji wa kafara. Hesabu 28:11, 10:10, Zaburi 81:3 Zaburi 81:3 Pigeni panda mwandamo wa mwezi, Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu.

5. #SABATO: · Sasa hapa naomba tuwe makini kwa sababu, ndipo penye changamoto kubwa. Agano la kale kulikuwa na Sabato zaidi ya moja

· SABATO YA SIKU YA SABA./ Sabato kabla ya dhambi.

  1. NB: sabato ya siku ya saba, ilikuwepo kabla ya dhambi kuingia Duniani, na hivyo laiti Adamu na Hawa hawangetenda dhambi, Sabato ingeendelea tu kuwepo kwa sababu ni kumbukumbu ya Uumbaji wa Mungu
  2. Kutoka 20:11

Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

Na hivyo kifo cha Yesu kilikuwa ni kwa ajili ya dhambi, na sabato ya siku ya saba ilikuwepo kabla ya dhambi, na hivyo sabato haikuwa na kosa lolote kama, ilivyo katika Ndoa, kwa sababu ukiondoa sabato unatangaza kwamba Dunia haijaumbwa na Mungu, bali imeibuka.

SABATO BAADA YA DHAMBI: Kwa hiyo baada ya dhambi kuingia zikatokea sabato nyingine, zilizokuwa zinaambatana na utoaji wa kafara. · Sabato ya Nchi, sabato hii ilikuwa inaadhimishwa, kwa kulima shamba miaka 6, na unapofika mwaka wa saba, nchi ilikuwa inasherekea sabato.

  1. Mambo ya Walawi 25:2-5

Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika nchi niwapayo, ndipo hiyo nchi itashika Sabato kwa ajili ya Bwana. Panda shamba lako miaka sita, na miaka sita lipelee shamba lako la mizabibu, na kuyachuma matunda yake; lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa Bwana; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu.

Sabato hii iliambatana na utoaji wa kafara, ambapo kafara zilikuwa ni kivuli, au kielelezo cha Yesu.

· SABATO YA KILA SIKUKUU Sikukuu zote walizokuwa wanasherekea wana wa Israeli, zilikuwa ni SABATO, yaani hiyo sherehe haijalishi imeangukia jumatatu, jumanne au siku yoyote, basi siku hiyo ilikuwa inaitwa sabato

  1. Mambo ya Walawi 23:26-33

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtazitesa nafsi zenu; nanyi mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto……Itakuwa kwenu #sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtazitesa nafsi zenu; siku ya kenda ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hata jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu.

Kwa hiyo kila mwaka tarehe 10 mwezi wa 7, ilikuwa ni sabato haijalishi ni juma ngapi, bora mradi iwe tarehe 10/7

· SABATO YA KUSAMEHE MADENI Wapo watu walikuwa wanakopa lakini hawana uwezo wa kulipa madeni, hivyo ndani ya miaka 6, ndio mtu aliruhusiwa kudai madeni, lakini ukifika mwaka wa saba, ulikuwa ni SABATO, kwa wadeni kusamehewa madeni yao. #Kumbu 15:1-11

· SABATO YA KUACHILIA WATUMWA Watumwa wote walikuwa wanafanya kazi kwa miaka 6, ukifika mwaka wa saba, ilikuwa ni Sabato kwa watumwa kuachwa huru bila kutumikishwa. #Kutoka 21 :1-3

Sasa baada ya Yesu kuja baadhi ya watu hawakumwamini na hata hawakujua uthamani wa kifo chake pale msalabani bali walikuwa wanaendeleza zile kawaida za agano la kale ambazo zilikuwa ni kivuli. Na watu hawa wakafika hadi Kolosai, na wakaanza kuwafundisha watu kwamba

Ni lazima, Kupiga mawe wazinzi, Ni lazima Kupiga mawe wavunja sabato, Ni lazima kuadhimisha mwandamo wa mwezi. N lazima watu washerekee sikuu za upatanisho, Malimbuko NK Ni lazima watu waendelee kutoa sadaka za vinywaji Ni lazima kuadhimisha sabato za nchi NK,

Na ndipo sasa Paulo anapata habari juu ya hawa waalimu wa uwongo, na sasa Paulo anawaandikia Wakolosai kwamba #wasihukumiwe juu ya Mambo hayo maana yalikuwa ni Kivuli tu, bali yalikamilishwa kupita mwili wa Kristo pale msalabani.

  1. Waebrania 9:10

kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya.

Kwa hiyo ndugu zangu Paulo alipokuwa anasema mtu asiwahukumu juu ya #Sabato na #Vyakula, hakumaanisha kualalisha ulaji wa vitu najisi kama nguruwe, na wala aliposema mtu asiwahukumu juu ya Sabato hakumaanisha Sabato ile ya siku ya saba hapana, bali alikuwa anazungumzia sabato za nchi, sabato za sikuu NK. Maana sabato hizi ndo ziliambatana na utoaji wa kafara, ambapo kafara hizo zilikuwa ni kivuli cha Yesu ambaye ndiye kafara kuu.

Sabato ni moja ya Amri kumi za Mungu, na hivyo ikiwa sabato iliishia msalabani, basi ilibidi amri zote kumi ziishie msalabani, kwakuwa huwezi kusema kuwa 1. Kuwa na miungu ni Dhambi 2. Kuchonga sanamu ni Dhambi 3. Kutaja bure jina la Mungu ni Dhambi 4. Kuvunja Sabato #SIO Dhambi 5. Kuto waheshimu wazazi ni Dhambi 6. Kuua ni Dhambi 7. Kuzini ni Dhambi. 8. Kuiba ni Dhambi 9. Kusema uwongo ni Dhambi 10. Kutamani ni Dhambi

Jamani hebu ifike wakati tujiongeze sio kila kitu cha kushabikia wewe unadanganywa kwamba sabato walipewa Wayahudi. Je hizo amri nyingine 9, mbona walipewa hao hao Wayahudi, lakini mbona unazitunza.?

Unadanganywa kwamba Ukimpoke Yesu tayari hakuna haja ya kutunza sabato, kwa sababu Biblia inasema:

  1. Marko 2:28 Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.

Jamani aya hii haisemi Mwana wa Adamu ndiye Sabato. Hapana

Kuna kiunganishi “WA” kinachoonesha Yesu ndiye mmiliki au mwasisi wa Sabato, Ikiwa na maana kwamba kwa sababu yeye Yesu ni Mungu ndiye aliyeiweka sabato na niya kwake.

Mfano: nikisema Mimi Emanuel ndiye bwana “wa” hili shamba. Je kwa kauli hiyo inanifanya mimi Kuwa nyumba? Jibu ni Hapana, Bali kama una hitaji shamba mimi ndiye ninaye jua taratibu na mipaka yote ya Shamba kwa sababu ninalimiliki.

Kwa hiyo ndivyo ilivyo kauli ya Yesu, Anaposema Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato,Ana maana kwamba yeye ndiye anayejua usahihi wa sabato kwa sababu ni yake.

Na aya nyingine ni hii: #Mathayo 11:28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Wito wa Yesu hapa sio watu waache kupumzika siku ya sabato hapana, bali wanaoitwa hapa kupumzishwa ni wale wenye mizigo ya Dhambi, Nguvu za Giza, Magonjwa NK. ndio wanaoitwa wapumzishwe, Hiki ndicho kilichomleta Yesu Duniani, soma #Luka 4:18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Hivyo kupumzika siku ya sabato ni Matokeo ya kukombolewa, kutoka katika utumwa wa Dhambi. . Isaya 1:19-20 [19]Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; [20]bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya. . MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 10:39, 4 August 2024 (UTC)[reply]

je warumi 14 inamaana gani

[edit]

Warumi 14:5-7 Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu. Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake.

Nawasalimu katika jina la BWANA WETU YESU KRISTO:

Ikiwa kuna mafungu yanayowachanganya Wakristo wengi, pamoja na Waislamu, ni mafungu yanayotoka katika Nyaraka za mtume Paul, na ndio maana hata mtume Petro alitoa angalizo juu ya usomaji wa nyaraka za Paulo na akatoa onyo lifuatalo:

  1. 2 Petro 3:15-17

Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa; vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe. Sio Petro tu ndio anadai kwamba nyaraka za Paul ni ngumu, bali hata watu wengine pia wanasema nyaraka za Paul ni ngumu, Na Paul yeye mwenyewe anashuhudia kwamba watu wanasema nyaraka zake ni nzito/ ngumu: 2 Wakorintho 10:9-10 nisije nikaonekana kana kwamba nataka kuwaogofya kwa nyaraka zangu. Maana wasema, Nyaraka zake ni nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini ni dhaifu, na maneno yake si kitu. . Hivyo inabidi umakini mkubwa sana unapokutana na aya tata katika Nyaraka za Paul, pia ieleweke kwamba Nyaraka zote za Paul alikuwa anashugulika na kutatua migogo ya kiimani iliyokuwa inatokea ndani ya Kanisa baina ya washiriki, na pia alikuwa anashugulika na walimu wa uwongo waliokuwa wakiingiza mafundisho potofu ndani ya kanisa. Ikumbukwe kwamba makanisa yote ambayo Paul anayaandikia nyaraka ni makanisa ya watu waliokuwa na mchanganyiko baina ya Wayahudi na watu wa Mataifa, mengine yalikuwa ni machanga katika imani.

  1. Sasa kabla ya yote inabidi tuzingatie mambo yafuatayo ili tuweze kuelewa nyaraka za Paulo na vitabu vingine:

1. Waraka huo aliwaandikia watu gani? 2. Kulikuwa na changamoto gani ? 3. Alishughulika vipi na hiyo changamoto.

Kwa hiyo kwa utangulizi huo, naomba tuchungze baadhi ya hoja zinazo patikana katika Warumi 14. Miongoni mwa hoja ambazo hujengwa na baadhi ya wakristo katika kitabu hiki ni 1. Siku zote ni sawa, hivyo unaweza kuabudu siku yoyote ile. 2. Ikiwa mwenzako anakula nguruwe wewe kumnyoshea kidole. 3. Hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake.

Kama ambavyo nimetangulia kusema Kanisa la Rumi lilikuwa na mchanganyiko wa Wayahudi na Watu wa mataifa, Rumi ilifikiwa na injili na mitume baada ya Yesu kupaa mbinguni, watu wengi wa mataifa waliokuwa wakisali katika kanisa la Rumi na Korintho, mwanzo walikuwa ni wapagani, wakijihusisha na ibada za sanamu, na hivyo baada ya kuipokea injili waliachana na upagani. Hata hivyo changamoto zilizokuwa zinalikabili Kanisa la Rumi, ndizo changamoto zilizokuwa zinalikabili Kanisa la Korintho.

  1. CHANZO CHA MIGOGORO JUU YA CHAKULA:

Kwa sababu kanisa lilikuwa linajumuisha Wayahudi na Wamataifa, hivyo mgogoro ulikuwa kati ya waumini wa Kiyahudi na waumini wa kimataifa. Sasa hawa waumini wasio wayahudi zamani kabla ya kumpokea Yesu walikuwa Wanatoa sadaka kwa masanamu, kisha ile nyama ilikuwa inapelekwa Masokoni kwa ajili ya kuwauzia watu, lakini baada ya kumpokea Yesu wakaachana na ibada za sanamu, na hata nyama zilizokuwa zinauzwa masokoni wakawa hawanunui, kwa kuhofu zitakuwa zimeolewa sadaka kwa sanamu na hivyo watajitia unajisi ,matokeo yake wakawa wanakula mbogamboga tu. Na Baada ya Paul kupata habari hizo juu ya huo mgogoro na ndipo anaandika waraka huu kwa Warumi. Na anaanza kwa kusema:

  1. Warumi 14:1-2

Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake. Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.

Kwa hiyo Paul anawaambia mtu akiwa mdhaifu wa imani wamkaribishe, haijarishi anakula nyama au hali asihukumiwe kwa imani yake aliyonayo. Kwa sababu imani yake ameijenga kwa Mungu. Ndipo sasa mgogoro ukainuka kanisani Wakristo wa kimataifa wakaanza kuwaona Wakristo wa Kiyahudi wamepotoka maana wanakula nyama zilizotolewa sadaka kwa sanamu, na Wayahudi nao wakawa wanawaona Wakristo wa kimataifa wamepotoka kwa kutokula nyama.

Lakini waumini wa Kiyahudi kwa sababu wao walikuwa hawajui historia ya zile nyama zinazouzwa masokoni, wao wakawa wananunua na kula, mbaya zaidi wakawa wanakula mbele za waumini wapya tena ndani ya mahekalu ya sanamu, na Paul anatoa onyo kwa kwa wale wanaokula nyama kwa kusema kwa dhamili zao:

  1. Warumi 14:22

Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali.

  1. 1 Wakorintho 8:10
Kwa maana, mtu akikuona wewe uliye na ujuzi, umeketi chakulani ndani ya hekalu la sanamu, je! Dhamiri yake mtu huyo, kwa kuwa yu dhaifu, haitathibitika hata yeye naye ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu?
  1. 1 Wakorintho 8:7-8

Bali ujuzi huu haumo ndani ya watu wote; ila wengine kwa kuizoelea ile sanamu hata sasa hula kana kwamba ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu; na dhamiri zao, kwa kuwa dhaifu, hunajisika. Paul anawaonya wale waliokuwa wanajiona wapo imara katika imani kwamba si vizuri kufanya mambo hayo hadharani, itawafanya wale waumini wapya kudhoofika kiroho.

Hivyo ikawa waumini wakienda sokoni kununua nyama walikuwa wanaanza kuuliza kwa wauzaji je, hii nyama imetolewa sadaka kwa sanamu au la, Na ndio maana Paul anawaambia Kanisa la Korintho wakienda sokoni wasianze kuulizauliza kwamba nyama hii imetolewa sadaka kwa sanamu au la, bali anawaambia kwa sababu ya dhamili wanunue maana hawawezi ukapata majibu sahihi:

  1. 1 Wakorintho 10:25
Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri;

Lakini kama mtu dhamiri yake haimruhusu basi asile maana atakuwa anatenda dhambi:

  1. Warumi 14:23

Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.

Fikiria hata wewe mwenyewe hivi umeenda sokoni ukaanza kuuliza nyama hii ni kibudu? unamuuliza muuzaji Au nyama hii ni ya leo au ya jana? Unadhani atakupa majibu sahihi? Ni wachache sana watakao kwambia ukweli. Hata sisi wenyewe tunanunua nyama kwenye mabucha kwa sababu dhamiri zetu zinatutuma kwamba ni nyama sahihi, lakini kiuhalisia kuna nyama nyingi haramu zinauzwa katika mabucha na wengi tumezila, hata nyingine ni za matambiko. Isitoshe vipo vyakula vingi tunavyokula sasa na tuna vipenda, ambavyo laiti tungejua mazingira na jinsi vinavyo tegenezwa hatungependa kula vile vyakula. Au ni mara ngapi umekula nyama ambayo hujui ni aina gani ya nyama au ni aina gani ya ndege?

Sasa hawa ndugu zetu wa Rumi na Korintho wakienda sokoni au wakialikwa mahali kwa mtu au katika sherehe, swali la kwanza walikuwa wanawauliza wahusika je, nyama hii imetolewa sadaka kwa sanamu? Wakiambiwa ndio basi hawali ile nyama..

Hivyo chanzo cha mgogoro ni juu ya ulaji wa nyama zilizo tolewa kafara kwa sanamu, ni makosa makubwa kutumia sura hii kuharalisha ulaji wa nguruwe, maana sio kiini cha mgogoro. Na haimaye Paul anatoa ushauri katika nyaraka zote mbili kwamba ni bora kuachana na ulaji wa nyama, ambao unasababisha migogoro ndani ya kanisa;

  1. Warumi 14:21
Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lo lote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa.
  1. 1 Wakorintho 8:13 Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu.
  1. CHANZO CHA MGOGORO JUU YA SIKU:

Naomba nirudie tena kusisitiza kwamba Paul anaandika waraka huu kutatua migogoro ya waumini waliomo ndani ya kanisa, na sio mgogoro kati ya dhehebu na dhehebu hapana, na ndio maana anasema katika:

  1. Warumi 14:1-2

Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake.

Kuonesha kwamba mgogoro ulikuwa kati ya watu wa imani moja, kama siku ya ibada walikuwa wanasali siku moja. Kwa sabubu Wayahudi wao walikuwa wanajiona ndio wazoefu sana katika imani, basi yapo mambo ambayo walkuwa wanataka kuwalazimisha, wenzao ambao ni wachanga wa imani ili watii, kile wanacho kiona wao chema. Wayahudi wengi walikuwa na ratiba zao za maombi na kufunga kulingana na siku walizojipangia, utakumbuka hata ule mfano wa Farisayo na Mtoza ushuru. Farisayo katika maombi yake alisema hivi:

  1. Luka 18:12

Mimi nafunga mara #mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. Hivyo Wayahudi walikuwa na siku maalumu za kufunga, na wanapoona watu wengine hawafungi, walikuwa wanajisikia vibaya. Na ndio maana siku moja baada ya wao kufunga lakini wanafunzi wa Yesu hawakufunga ikabidi wapeleke mashtaka kwa Yesu juu ya wanafunzi wake kuto kufunga.

  1. Mathayo 9:14-15

Wakati ule wanafunzi wake Yohana wakamwendea, wakasema, #Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga, bali wanafunzi wako hawafungi? Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga. Na ndio maana Yesu aliwakemea kwa tabia yao ya kufunga kwa maonesho.

  1. Mathayo 6:16-17

Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;

Kwa hiyo hata katika kanisa la Rumi kulikuwa na watu walioweka siku zao maalumu za kufunga, na wakawa wanataka kanisa lote lifuate mfumo wao, na ndipo Paul anasema:

  1. Warumi 14:5-7

Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana.

Kuna mambo mengine ni ya Kanisa na mengine ni ya mtu binafsi, suala kufunga ni hitaji na mguso wa mtu binafsi na sio la kulazimishana, kuna watu wengine mwaka mzima unaisha hajawahi kufunga hata siku moja na mwingine akisikia tu ratiba ya kufunga na kuomba anaanza kuumwa vidonda vya tumbo. Sasa huwezi ukawalazimisha watu kufunga, na haujui ratiba zake yeye za maombi zipo vipi.

  1. NB: Paulo hasemi yeye #AFANYAYE IBADA hufanya kwa Bwana hapana, Bali anasema yeye #AADHIMISHAYE siku, .

Pia kulikuwa kuna watu walikuwa wanaadhimisha baadhi ya siku kukumbuka matukio yao binafsi, yasio husiana na utaratibu wa mfumo wa kanisa. Kwa hiyo ni vibaya kutumia Warumi 14 kutetea ibada ya jumapili, maana sio kiini cha mada.

  1. HAKUNA KITU KILICHO NAJISI KWA ASLI YAKE
  1. Warumi 14:14-15

Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.

  1. >>>>Watu wengi hupenda kutumia fungu hili kama kichaka cha kutetea ulaji wa nguruwe hasa katika kipengele kinachosema>>> #Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake.

Kwa hiyo kama nilivyotangulia kusema hoja katika sura hii sio ulaji wa nguruwe, bali ni ulaji wa nyama zilizotolewa kafara kwa sanamu, na ulaji wa mbogamboga.

Lakini pia Paul anapoandika aya hii anaandika kulingana na tukio na mazingira, Anaposema #Hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake# Kauli hii anazungumza na Kanisa la Rumi kulingana na mgogoro uliokuwepo kwa sababu hakuna mnyama yeyote najisi ambaye huwa anatolewa sadaka kwa sanamu wala huwezi kusikia mganga wa kienyeji amedai mtu apeleke nguruwe, mbwa, paka, au bata kwa ajili ya kafara kwa miungu yake. Wanyama ambao hutolewa sadaka iwe kwa sanamu au kwa waganga ni wale ambao ni safi: kama ng’ombe, mbuzi, kondoo nk.

Hivyo basi Paul anaposema #Hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake# alikuwa anamaanisha wale wanyama waliokuwa wanatolewa sadaka hapo Rumi yaani kama mbuzi, kondoo, ng’ombe nk.. kwa sababu ni wanyama safi, tangu asili yake, hivyo hawawezi wakawa najisi, labda kwa mtu binafsi.

Mfano; ukija kwangu mimi emanuel nikikwambia uwe huru kula nyama yoyote maana ni safi, kwa kauli hiyo sina maana ya nyama ya nguruwe, kobe, sungura nk. Sasa hii ni kauli ya kimazingira kulingana na imani yangu ina maana ya nyama ya mbuzi, kondoo, kuku, nk. Kwa hiyo huwezi ukatumia kauli hiyo kudai kwamba emanuel anakula nguruwe au sungura. Au nime halalisha ulaji wa nguruwe hapana.

Hata hivyo Paulo anahitimisha hoja yake ya kutatua mgogoro kwa kuwahimiza Waumini wa Kiyahudi kwamba wajitahidi kuonesha upendo kwa waumini wa Kimataifa, na sio wao Wayahudi kujipendeza wenyewe:

  1. Warumi 15:1-2

Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe. Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe.

Ukweli ni kwamba Warumi sura ya 14,haina uhusiano wowote na suala la ibada ya siku ya saba au siku ya kwanza ya juma, na wala haitetei wala kupinga ulaji wa wanyama najisi. MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 10:40, 4 August 2024 (UTC)[reply]

JE, WEWE NI MOJA WAPO YA MASKINI WA ROHO?

[edit]

heli leo mwisho wa somo hili tuchague utajili au umaskini wa Roho

Maskini ni mtu ambaye ni muhitaji wa jambo fulani(kitu) ambacho yeye hana au amepungukiwa. Kwa kawaida maskini kwa sababu ni muhitaji, basi huwa anakuwa mnyenyekevu na mtiifu kwa kile anachagizwa au kuambiwa na yule anayempa msaada.

Sasa Yesu anasema: Mathayo 5: 3 Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Kama ambavyo katika ulimwengu wa mwili kuna matajiri na maskini, ndivyo hata katika ulimwengu wa kiroho kuna matajiri na maskini. Sasa Yesu anasema heli ambaye ni maskini wa Roho maana huyo atauona Ufalme wa Mungu.

Maskini wa Roho ni mtu ambaye wakati wote yeye ni muhitaji wa Neno la Mungu, yaani kila wakati anajiona anahitaji msaada wa kiroho kutoka kwa Bwana wake(Yesu) na hivyo kwa sababu wakati wote anahitaji msaada na anakuwa mnyenyekevu, basi Bwana wake ni lazima atampa kile anachohitaji. Maskini wa roho ni mhangaikaji na wala hatulii wala halidhiki na alicho nacho, wakati wote anautafuta ukweli ni upi ili awe huru.

Maskini wa roho anaomba kila wakati na wala hakati tamaa ili apate chakula cha kiroho na aujue ukweli zaidi. Luka 18 :1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.

Katika mambo ya kiroho ukiona mtu anajiona yeye ni bora kuliko wengine, au anajiona yeye ni Mtakatifu sana kuliko wengine, basi hiyo ni dalili ya kuwa tajiri, ambayo ni ishara mbaya. Au ukiona mtu hana haja ya kuuchunguza ukweli wa Neno la Mungu basi huyo ni tajiri.

Tajiri wa kiroho anaridhika na kile alichonacho hata kama ni mapokeo, tajiri wa kiroho wakati fulani hataki kusikia jambo lolote jipya nje ya kile anachokijua.

Tunapaswa wakati wote tuwe maskini wa roho ili Mungu atupatie kile tunachokihitaji. Na ikiwa tunautafuta ukweli wa Neno la Mungu, basi hatuna budi kuwa maskini wa kiroho, kwa kulichunguza Neno la Mungu.


MUNGU ATUBARIKI TUNAPOJIANDAA KUWA MASKINI WA KIROHO 🙏🙏🙏🙏

  • tafadhali sambaza kwa wengine* 🙏🙏🙏🙏

MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 10:42, 4 August 2024 (UTC)[reply]

HASARA KUBWA kwa wale wote wanaozikataa KUTII AMRI KUMI ZA MUNGU

[edit]
  • HASARA KUBWA kwa wale wote wanaozikataa KUTII AMRI KUMI ZA MUNGU zile za akina usiibe, usiue, ikumbuke siku ya sabato, usizini, usiabudu miungu wengine nk*
  • BIBLIA INATAJA MADHARA YA KUZIKATAA AMRI NA SHERIA*
  • ZA MUNGU.*

1.WANAOKATAA AMRI ZA MUNGU, WANAFANYA IBADA YA BURE.

"Nao waniabudu bure wakifundisha Mafundisho yaliyo maagizo ya Wanadamu. Ninyi mwaiacha AMRI ya MUNGU , na kuyashika mapokeo ya Wanadamu." (Marko 7:7,8) "Akajibu, akawaambia, mbona ninyi nanyi HUIHALIFU AMRI YA MUNGU kwa ajili ya mapokeo yenu? ...Nao waniabudu bure, wakifundisha Mafundisho yaliyo maagizo ya Wanadamu." (Mathayo 15:3,9)

2.WASIOSHIKA AMRI ZA MUNGU WANAHESABIWA KUWA WAONGO.

"Yeye asemaye, nimemjua, wala hazishiki Amri zake, ni MWONGO wala kweli haimo ndani yake." (1Yohana 2:4) "Umewakataa wote wazikosao amri zako kwa maana hila zao ni UONGO." (Zaburi 119:155)

3. ANAYEVUNJA AMRI MOJA KATI YA AMRI KUMI HUHESABIWA KAVUNJA ZOTE KWA KUWA AMRI ZOTE ZILITOKA KWA MUNGU.

"Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, AMEKOSA JUU YA YOTE. Kwa maana yeye aliyesema, usizini, pia alisema, usiue, Basi ujapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria." (Yakobo 2:10,11)

4.YESU ANASEMA NI UNAFIKI KULIPA ZAKA NA KUACHA MAMBO MAKUU YA SHERIA. "Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya SHERIA, yaani, adili,na rehema,na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache." (Mathayo 23:23)

5.MUNGU ANAWAKATAA WAVUNJA AMRI ZAKE.

"Umewakataa wote wazikosao amri zako, kwa maana hila zao ni uongo." (Zaburi 119:118)

6.WASIOJIFUNZA AMRI ZA MUNGU, WOKOVU UKO MBALI NAO.

"Wokovu u mbali na wasio haki, kwa maana hawajifunzi amri zako." (Zaburi 119:155)

7. WANAOKATAA AMRI ZA MUNGU; MUNGU ATAWAPA ADHABU.

"Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Yuda, naam , kwa manne, sitazuia ADHABU yake isimpate; kwa sababu WAMEIKATAA SHERIA YA BWANA; wala HAWAKUZISHIKA AMRI ZAKE ; na maneno yao ya uongo yamewakosesha, ambayo baba zao waliyafuata." (Amosi 2:4)

8.BWANA ANAWAGHADHIBIKIA SANA WAZIACHAO SHERIA NA AMRI ZAKE.

"WAKAZIACHA AMRI ZOTE ZA BWANA, Mungu wao...Kwa hiyo BWANA AKAWAGHADHIBIKIA Israeli sana, akawahamisha mbali na uso wake, wala hapana aliyesalia ila kabila ya Yuda peke yake." (2 Wafalme 17:16,18) "Ghadhabu imenishika kwa sababu ya wasio haki, waiachao sheria yako." (Zaburi 119:53) "Naam, walifanya mioyo yao kuwa kama jiwe gumu, wasije wakaisikia Sheria na maneno ya BWANA wa Majeshi, aliyoyapeleka kwa roho yake kwa mkono wa manabii wa kwanza, kwa sababu hiyo GHADHABU KUU Kutoka kwa BWANA wa majeshi." (Zekaria 7:12)

9. ANAYEACHA AMRI ZA MUNGU ANAMFUATA MUNGU BAALI NA NI MTAABISHAJI WA WATU WA MUNGU.

"Naye akajibu, si mimi niliyewataabisha Israeli; bali ni wewe, na nyumba ya baba yako, kwa kuwa mmeziacha amri za BWANA; nawe umefuata mabaali." (1 Wafalme 18:18)

10.ASIYETAKA KUISIKIA SHERIA HATA SALA YAKE NI CHUKIZO KWA MUNGU.

"Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, hata sala yake ni chukizo." (Mithali 28:9)

11.WASIOTAKA KUISIKIA SHERIA YA MUNGU BIBLIA INAWAITA WAASI.

"Kwa maana watu hawa ni watu WAASI, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya BWANA." (Isaya 30: 9)

12. WASIOENDA KWA SHERIA NA USHUHUDA HAWAMA ASUBUHI - (WAKO GIZANI) "Na waende kwa sheria na Ushuhuda, ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi" (Isaya 8:20)

Lakini kwa ufupi tu kuhusu amri za MUNGU zinachukua sehem gani katika uzima wetu wa milele waweza tazama somo hili MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 10:43, 4 August 2024 (UTC)[reply]

JE, WANAOABUDU JUMAPILI WATAPOTEA??

[edit]

🤔🤔🤔🤔

  1. SWALI LA WATU WENGI: JE, WANAOABUDU JUMAPILI WATAPOTEA:

Kati ya hoja ambazo ndugu zangu wanaoabudu jumapili wamekuwa wakihoji ni pamoja na: 1. Je, wanaoabudu jumapili Mungu atawaangamiza? 2. Ikiwa kuabudu siku ya sabato ni muhimu, mbona wanaoabudu jumapili wakiomba maombi yao kwa Mungu wanajibiwa na wanatendewa miujiza? 3. Ikiwa wanaoabudu jumamosi wapo sahihi, itakuwaje Mungu awaangamize mamilioni ya watu wanaoabudu jumapili na ijumaa, halafu aokoe kundi dogo la wanaoabudu siku ya sabato?

Hayo ni baadhi ya maswali ambayo nimekuwa nikikutana nayo kutoka kwa baadhi ya ndugu zangu wanaoabudu jumapili, naamini hata wewe umekutana nayo au una maswali kama hayo ndugu mpendwa. Sasa kabla hatujajibu swali letu kuu, hebu tujibu kwa ufupi swali la 2 na 3,

Suala la kujibiwa maombi haina maana upo sahihi kwa mujibu wa Biblia, bali upo sahihi kwa mujibu wa Nuru uliyopewa na kile unachokiamini. Mungu anaweza kujibu maombi ya mtu yeyote Yule haijalishi dini au dhehebu, ijapokuwa wakati fulani anachokiamini ni kinyume na mapenzi yake. Lakini anamjibu kwa sababu bado hajapewa Nuru ya kweli. Lakini pia Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote Yule kufikisha ujumbe hata kama ana madhaifu.

  1. Mfano: Kornelio hakuwa Muisraeli, bali alikuwa Mrumi na wala hakuwa amebatizwa na wala alikuwa hamuamini Yesu, lakini Ibada aliyokuwa anaifanya ijapokuwa kimakosa na katika udhaifu Mungu aliipokea sala zake na hata maombi yake yalipokelewa , lakini alihitaji kupewa Nuru zaidi.

Matendo ya Mitume 10:1-4 Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima. Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio! Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.

Yakobo 4:17 Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.

Mungu hawezi kumuhukumu mtu au kutokujibu maombi yake endapo mtu huyo hajapewa Nuru ya kuonesha kosa kwa kile anachokifanya, yaani Mungu hawezi kushindwa kumjibu mtu maombi kwa sababu anasali jumapili au ijumaa, wakati mtu huyo bado hajajua kwamba kuabudu jumapili ni makosa. Lakini mtu akishafunuliwa Nuru na akajua kabisa kwamba siku ya ibada ni jumamosi lakini yeye akashupaza shingo, hapo ndipo pana shida. Mungu ameruhusu nuru ya sabato kuhubiriwa kila mahali ili watu waliokuwa wamepofushwa wapate nuru, na siku ya mwisho asiwepo mtu wa kutoa udhuru kwamba sikusikia.

Lakini pia suala la kujibiwa maombi na kutoa pepo na kutenda miujiza inabidi tuwe makini sana kwa sababu ndio kigezo kikubwa anachotumia shetani kupoteza watu katika nyakati hizi, ushirikina na uchawi umeingizwa makanisani kwa kigezo ni miujiza: Mathayo 24:24-25 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele.

Mathayo 7:21-23 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

Kwa hiyo shetani naye ana uwezo wa kukujibu maombi hata kama unalitaja jina la Yesu, lakini kama haufuati maagizo ya Mungu shetani atakujibu maombi maana upo upande wake. Hebu fikiria wachawi nao wanaiomba mizimu yao na wanajibiwa, vyama vya siri kama Freemason wanaiomba miungu yao wanajibiwa, na wengine wamefungua makanisa kabisa na jina la Yesu linatajwa, lakini kwa unafiki kama mwavuli wa kusitiri uovu wao.

Na hoja ya wingi au uchache: Hili ni kwamba suala la wengi wape, haya ni mambo ya siasa wapendwa na sio mambo ya Mungu, mambo y

a siasa ni kwa

mba ikiwa imepigwa kura juu ya hoja ya Ushoga, kama wengi wakikubali kwamba wanataka ushoga basi unapita bila shida, Lakini mambo ya Mungu sio wengi wape Bali wanaotii ukweli wa Neno la Mungu wape haki yao hata kama ni mmoja. Kwa hiyo katika suala la wokovu Mungu haangalii uwingi wa watu wanaoangamia, bali anaangalia ni uaminifu, maana kama wokovu ni kuangalia uwingi, basi 1. Kipindi cha Nuhu hawangeokolewa watu 8 na kuangamizwa maelfu ya watu.Mwanzo 9:18 2. Kipindi Sodoma na Gomora hawangeokolewa Familia ya Lutu peke yake na kuangamizwa maelfu ya watu.mwanzo 19 3. Kipindi cha Taifa la Israel wanaume wenye umri zaidi ya miaka 20, ambao pia walitoka Misri waliangamia jangwani na Yoshua na Kalebu peke yao ndio waliingia Kanani. Hesabu 14. Mungu anasema hata kama kuna watu watatu tu wenye haki haohao atawakoa kwa sababu ya haki waliyo nayo: Ezekieli 14:14 wajapokuwa watu hawa watatu, Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kuwamo ndani yake, wangejiokoa nafsi zao wenyewe tu kwa haki yao, asema Bwana MUNGU.

Kwa hiyo ndugu yangu usiangalie uwingi wa watu, bali angalia Mungu anakutaka wewe ufanye nini ili uokolewe Sasa kulingana na hoja ya somo letu linalohoji kwamba Wanaoabudu jumapili watapotea? Au lah!1!! Tuseme kwamba kazi ya mwanadamu ni kuhubiri injili ya kweli ili watu waokolewe, lakini suala la kuchora mstari wa hukumu sio kazi yetu hiyo ni kazi ya Mungu peke yake kwa sababu Mungu ana watu wake katika kila Dhehebu na kila Dini ambao ni waaminifu, ijapokuwa bado hawajapata Nuru ya kweli. Mstari wa utengano kwa wanaoabudu jumapili utakuja kuchorwa baadaye baada ya injili kuhubiliwa kwa kila mtu na watu wakakataa, na jumapili ikapitishwa kama siku ya ibada na watu wakaipokea kama siku ya ibada kwa kukataa kwa makusudi kabisa Ibada ya Biblia ya siku ya sabato, na hii ndio Chapa ya Mnyama, Ufunuo 13:15-18. lakini kwa sasa Mungu bado anatenda kazi ya kuwaangazia nuru watu wake kutoka kila Dini na dhehebu, na waaminifu wanatoka.

Lakini wewe mwenyewe ndio unaweza ukajihoji pia na kupata majibu kwamba unaweza kuokolewa au kupotea kwa kuabudu jumapili lakini sio usemewe na mtu maana majibu yapo wazi, kwa sababu hoja ya sabato ni moja ya Amri Kumi za Mungu, na kila dhehebu linaamini uwepo wa Amri 10, sasa jiulize haya maswali juu ya amri 10 kisha ujijibu. na kama unapoabudu haufundishwi kwamba sabato ni moja ya amri ya Mungu basi utambue hilo leo kwamba unapotezwa. maana sabato ni amri ya 4 kati ya zile amri 10. sasa jiulize maswali haya kisha ujiulize swali je wanaoabudu jumapili siku ya mwisho wataokolewa au la!!!! 1. Je, mtu anayeabudu miungu mingine ataenda mbinguni? 2. Je, mtu anayeabudu sanamu ataenda mbinguni? 3. Je, mtu anayelitaja jina la Mungu ovyo ataenda mbinguni? 4. Je, mtu anayevunja sabato ataenda mbinguni? 5. Je, Mtu akiwadharau wazazi wake ataenda mbinguni? 6. Je, muuaji ataenda mbinguni? 7. Je, mtu anayezini ataenda mbinguni? 8. Je, mtu anayeiba mali za watu ataenda mbinguni? 9. Je, mtu anayesema uongo ataenda mbinguni? 10. Je, mtu anayetamani mali za watu au mke wa mtu ataenda mbinguni?

Sasa jiulize hivi Mungu anaweza akawahukumu watu wanaovunja amri 9, na akawaacha wanaovunja amri moja ya 4? Je huoni kwamba huo ni upendeleo ikiwa mzinzi au mwizi atahukumiwa kwa sababu amevunja amri ya Mungu, sasa kwanini anayevunja amri ya 4 ya sabato aachwe? Yakobo 2:10-11 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria.

mwingine atasema amri ya sabato walipewa Waisrael: ukweli ni kwamba Amri zote 10 walikabidhiwa waisraeli, kwa hiyo kama ni hoja ya kupewa waisraeli basi inabidi uvunje amri zote 10, kama kuiba we iba kama kuzini we zini kama kuua we ua kama kuvunja sabato we vunja kama kusema uongo we sema nk maana amri hizi kumi walipewa waisrael

Kwa hiyo kama unataka kurithi ufalme wa Mungu tii amri zote 10 ikiwemo ya sabato ambayo ni Amri ya 4: Mathayo 19:17 Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.


MUNGU AKUBARIKI MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 10:44, 4 August 2024 (UTC)[reply]

siku ya BWANA ni ipi??

[edit]
  • nalikuwa katika ROHO SIKU YA BWANA ...........* UFUNUO 1:10 👈👈👆👆👆👆👆 kwa andiko hili linaonyesha kuwa *MUNGU WA MBINGU NA NCHI* ANASIKU YAKE Takatifu lakini pia hata ukisoma fungu hili isaya 58:13,14 """"""kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, *usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu*, ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima.............."""" 👈👈👆👆 kwa fungu hili inaonesha kuwa siku ya sabato inamaana kubwa sana katika ulimwengu wa ROHO lakini kibinadam siku zote ni sawa tu. kwa kuwa MUNGU ni ROHO basi wamwabuduo katika ROHO na kweli wataelewa umuhimu wa sabato yake lakini hata YESU MWENYEWE alisema """ *mwana wa adam (YESU) ndiye BWANA wa sabato*""" malko 2:28 kwa hiyo kama mwana wa hamisi (juma) ndiye bwana wa harima au mwana wa john (kefa) ndiye bwana wa shamba hili. kwahiyo kama juma mwana wa hamisi alivyo mmiliki wa harima au kama kefa mwana wa john alivyo mmiliki wa shamba basi *vivyo hivyo YESU KRISTO NDIYE MWENYE HIYO SIKU YAKE TAKATIFU YA SABATO* kwa hiyo anatusihi *ikumbuke siku ya sabato na uitakase* kutoka 20:8 pia mitume kwa heshima kuu waliitunza hiyo siku ya BWANA matendo ya mitume 16:13 *hata siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusalia; tukaketi tukasema na wanawake waliokutana pale*

kwa hiyo mpendwa kila ikifika siku ya sabato basi tafuta mahali pa kusalia (kufanyia ibada siku yote)

.

  • tafadhali shera kwa wengine nao wakumbushwe kuhusu hii siku ya Bwana*

Mpaka hapa ni maamuzi yako. Kuitunza au kuto itunza siku takatifu ya Bwana

.😍😍😍😍😍😍

  • share to other (sabaza kwa wengine)*

😍😍😍😍😍😍

  • ubalikiwe sana unapo fanya bidii kuitii na kuikumbuka siku takatifu ya Bwana*

🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏 MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 10:45, 4 August 2024 (UTC)[reply]

MADHEHEBU MENGI KIPINDI CHA YESU HAUKUWA MPANGO WA MUNGU, NA HATA SASA SI MPANGO WA MUNGU.

[edit]

MAFUNGU MAKUU:"...1. "tena ni kichwa cha madhehebu ya Wanazorayo." (Matendo 24:5) 2. ... hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo ... (Matendo 5:17) 3. " ya kwamba nalikuwa Farisayo kwa kuifuata madhehebu ya dini yetu..."

     (Matendo  26:5)

Biblia inataja Madhehebu Mengi yaliyokuwapo kipindi cha Yesu. Baadhi ya Madhehebu hayo yalikuwa:

1. DHEHEBU LA MASADUKAYO. . " Akaondoka Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo),.."(Matendo 5:17)

2. DHEHEBU LA MAFARISAYO.

" wakinijua sana tangu mwanzo, kama wakipenda kushuhudia, ya kwamba nalikuwa Farisayo kwa kuifuata madhehebu ya dini yetu iliyo sahihi kabisa." (Matendo  26:5)

3. DHEHEBU LA WANAZORAYO.

 " Kwa maana tumemwona mtu huyu mkorofi, mwanzilishi wa fitina katika Wayahudi wote duniani, tena ni kichwa cha madhehebu ya Wanazorayo.    (Matendo 24:5).  

Yalikuwapo pia madhehebu mengine zaidi ya Waeseni, Mahedi nk lakini Biblia imeyajadili kwa undani zaidi madhehebu ya Wanazorayo, Masadukayo na Mafarisayo. Tutaangalia madhehebu haya matatu kama msingi wa somo hili.

1. DHEHEBU LA WANAZORAYO. Hili ndilo lilikuwa dhehebu la BWANA YESU. " Yesu aliitwa Mnazorayo" "akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo. (Mathayo 2:23)

Baadaye Wanazorayo walianza Kuitwa WAKRISTO kule Antiokia. (Matendo 11:26) Dhehebu hilo la Wanazorayo PAULO aliliita KANISA LA MUNGU. (Wagalatia 1:13; Wafilipi 3:6) Dhehebu hili ndilo Yesu alilianzisha na kuliita kanisa lake, kundi lake, zizi lake nk.

"Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. " (Mathayo 16:18) Mpango wa Yesu ni kuwakusanya wateule wake wote katika zizi/kundi/ kanisa lake kutoka katika madhehebu mengine. " Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja." ( Yohana 10:16) Mafundisho makuu ya dhehebu hili ni Imani katika Yesu, Kushika amri za Mungu, matukio ya siku za mwisho, ubatizo wa maji mengi, kutunza sabato, hali ya wafu na ufufuo, Ukuhani wa Yesu mbinguni nk. Paulo alishutumiwa kuwa kichwa (kiongozi) cha Wanazorayo baada kuhama kutoka dhehebu la Mafarisayo. " Kwa maana tumemwona mtu huyu mkorofi, mwanzilishi wa fitina katika Wayahudi wote duniani, tena ni kichwa cha madhehebu ya Wanazorayo." ( Matendo 24:5) Kimsingi, migawanyiko ya Dini, makanisa na madhehebu imesababishwa na kuhitilafiana katika mafundisho ya imani. Kukosekana kwa mafundisho yanayofanana kumesababisha ziwepo imani nyingi, dini nyingi, makanisa mengi, na madhehebu mengi. Biblia inasema kuukataa ukweli ndiyo sababu kuu ya kuwapo kwa madhehebu. Biblia inasema kwa kukataa mafundisho yenye uzima na kukumbatia mafundisho ya uongo ndiyo chanzo cha utitiri wa makundi ya kimadhehebu. Imeandikwa: "Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; (2 Timotheo 4:3) Kanisa la korintho liligawanyika kutaka kuunda makundi, Paulo akaukemea mgawanyiko huo kwa maneno makali. "Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo. Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo? " (1 Wakorintho 1:11-13) Kanisa la Mungu ndilo mwili wa Kristo. Kristo ana mwili mmoja usiogawanyika. "Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja. " (1 Wakorintho 12:13) Roho wa Kristo anayekaa rohoni mwa watu wa dhehebu moja hatagombana na Roho wa Kristo anayekaa kwa watu wa dhehebu jingine na kushindwa kuwaunganisha. Roho huyo mmoja akiyaongoza madhehebu yote, madhehebu hayo hayawezi kuwa na imani tofauti tofauti kama ilivyo leo. Kuna wanaoamini Bikira Maria ndiye mwombezi wetu huku wengine wakipinga vikali, Kuna wanaopinga Sabato na sheria za Mungu, Wengine wanasema Sabato ni amri halali ya Mungu. Kuna wanasema Mohammedi ni mtume wa Mungu huku wengine wakimkataa. Ni wazi kuwa Dini na madhehebu yote hayaongozwi na Mungu yule yule mmoja. Ikiwa mapenzi ya Mungu yamepokelewa na Wakristo wote tunawezaje kuhitilafiana na kutengana kiimani na kimafundisho? Biblia inasema Msingi wetu ni mmoja tu, unaoundwa na Mitume, manabii na Kristo Yesu mwenyewe. "Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. " (Waefeso 2:20) Juu ya msingi huu huu watu wote tunapaswa kujengwa pamoja kuwa hekalu (kanisa) moja la Mungu. "Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho. (Waefeso 2:22). Biblia inasema tunapaswa kuwa na imani moja tu, yaani kanisa moja tu kwa watu wote. "Bwana mmoja, IMANI MOJA, ubatizo mmoja." (Waefeso 4:5) Kanisa la Agano la kale kwa miaka mingi lilikuwa kanisa moja likiwa pia taifa takatifu la Israeli. "Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi. " (Matendo ya Mitume 7:38)

YESU ANAKUBALIANA NA UWEPO WA MADHEHEBU MENGI? "Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si kwa sababu ya mkate naliwaambia? ILA JILINDENI NA CHACHU YA MAFARISAYO NA MASADUKAYO. Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na MAFUNDISHO YA MAFARISAYO NA MASADUKAYO." (Mathayo 16:11,12) Yesu aliyapinga vikali Madhehebu pinzani ya wakati wake, yaani dhehebu la Mafarisayo na Masadukayo; na mafundisho yao; akayatangazia anguko la kiroho. Hivyo watu wengi waliyahama Madhehebu hayo kufuata injili ya kweli ya Bwana Yesu na mitume wake. Mfano mzuri ni Paulo ( Sauli) aliyekuwa katika dhehebu la Mafarisayo, baada ya kutokewa na Yesu alihamia dhehebu la Wanazorayo waliokuja kuitwa Wakristo kule Antiokia. Barnaba alimtwaa Paulo na kumpeleka kwa Mitume waliokuwa ndio viongozi wa kanisa la Mungu wakati huo, nao wakampokea. "Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi. Lakini Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ushujaa katika Dameski kwa jina la Yesu.

Naye akawa pamoja nao katika Yerusalemu akiingia na kutoka." (Matendo  9:26-28)

DHEHEBU LA MASADUKAYO WALIKUWA NA SHIDA GANI KATIKA MAFUNDISHO YAO?

"Kwa maana Masadukayo husema ya kwamba hakuna kiyama wala malaika wala roho; bali Mafarisayo hukiri yote. (Matendo 23:8) "Kisha baadhi ya MASADUKAYO wakamwendea, wale wasemao ya kwamba HAKUNA UFUFUO..." (Luka 20:27).

Hawa walipinga Fundisho la YESU la Ufufuo. (Yohana 5:28,29; Yohana 6:39,40,44,54 ; Yohana 11:1-56), Walipinga uwepo wa malaika na uwepo wa roho.

Kilichosababisha Masadukayo kupinga fundisho la ufufuo na uwepo wa malaika ni upofu wa maandiko na kutowaamini manabii waliotangulia kwa sababu fundisho la ufufuo lilikuwa tayari wanalo katika chuo (kitabu) cha nabii isaya na nabii Daniel. Isaya alifundisha akisema: "Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; ...nayo ardhi itawatoa waliokufa. " (Isaya 26:19) Daniel alithibitisha uwepo wa malaika Gabriel" (Daniel 9:21), na ufufuo wa wafu (Daniel 12:2) Wapo wengi hivi leo wasiopenda kusikia maandiko ya Agano la kale ya manabii; Kama Masadukayo, nao wanatembea gizani wakipinga mafundisho yaliyo jaa ukweli wote.

DHEHEBU LA MAFARISAYO WALIKUWA NA SHIDA GANI KATIKA MAFUNDISHO YAO?

YESU ALIWAAMBIA MAFARISAYO:
"Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami;  Nao waniabudu bure, WAKIFUNDISHA MAFUNDISHO yaliyo maagizo ya wanadamu,  NINYI MWAIACHA AMRI YA MUNGU, na kuyashika mapokeo ya wanadamu. Akawaambia, Vema! MWAIKATAA AMRI YA MUNGU mpate kuyashika mapokeo yenu. " (Marko 7:5-9)

"Ninyi mwaiacha AMRI YA MUNGU...., Nao WANIABUDU BURE WAKIFUNDISHA MAFUNDISHO YALIYO MAAGIZO YA WANADAMU" (Marko 7:1,8,7) " Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini MMEACHA MAMBO MAKUU YA SHERIA, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. (Mathayo 23:23) Mafarisayo walikuwa WAMEACHA AMRI NA SHERIA ZA MUNGU, Yesu akawakemea vikali. Kuiacha amri yoyote ya Mungu ni kufanya ibada ya bure kabisa. Angalia katika Orodha ya amri kumi (Kutoka 20:3-17); ukiona kuna amri umeicha, na kanisa lako hawaishiki, dawa ni kuondoka huko mapema kama Paulo alivyohama kutoka kwa Mafarisayo. Yohana mbatizaji naye aliwaita Mafarisayo na Masadukayo wana wa nyoka; nyoka ni shetani. "Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?" (Mathayo 3:7)

WITO WA MUNGU NI KUTOKA KATIKA MADHEHEBU YALIYOKATAA MAFUNDISHO SAHIHI YA YESU.

"Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake." (Ufunuo 18:4) Leo hii utitiri wa madhehebu adui yao mkubwa ni amri za Mungu. Kama wewe ni mmoja wao, hauko salama, hama huko mapema kama Paulo alivyohama kutoka dhehebu la Mafarisayo na kujiunga katika dhehebu la Wanazorayo waliokuwa wanamwamini Yesu na kushika amri zake. PAULO anasema: "wakinijua sana tangu mwanzo, kama wakipenda kushuhudia, ya kwamba nalikuwa Farisayo kwa kuifuata madhehebu ya dini yetu iliyo sahihi kabisa. (Matendo 26:5) "Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, " (Wagalatia 1:15). Paulo alipoitwa, akatoka kwa Mafarisayo na kujiunga na Mnazorayo. "Kwa maana tumemwona mtu huyu mkorofi, mwanzilishi wa fitina katika Wayahudi wote duniani, tena ni kichwa cha madhehebu ya Wanazorayo. (Matendo 24:5) MUNGU AKUBARIKI SANA MSOMAJI WANGU MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE (talk) 10:50, 6 August 2024 (UTC)[reply]