Jump to content

User:MUNGU AZUNGUMZA NA WATU WAKE

From Wikipedia, the free encyclopedia


Historia fupi ya sherehe za mwaka mpya na asili yake

Kwanza kabisa tukumbushane katika hili

NB

Kila kinachoongelewa, kufanywa, kutendwa, kusherekewa au namna yoyote ile ambayo mwanadam anaishi ni ibada kwa MUNGU WA MBINGUNI au ibada kwa ibilisi shetani

Hivyo usinakili maisha anayo ishi mtu furani maana utaiabudu miungu isiyo kuhusu bali kua wewe kama wewe ukiongozwa na kweli ya biblia ambayo ndiyo asili ya mwanadam maana MUNGU ndiye asili yetu sisi wanadamu

Desturi ya kusherekea mwaka mpya hasa ilianzia huko Babeli Mesopotamia (kwa sasa ni Iraki) mnamo mwaka 2000 KK, wakati kabisa ambao mzee Ibrahimu alikuwa hai. Watu wa Mesopotamia waliadhimisha mwaka mpya katika kipindi cha Ikwinoksi ya majira vuli, katikati ya mwezi Machi wa leo. (rejea: Brunner, Borgna. “A History of the New Year” Infoplease.com. Retrieved 31 January 2014; na Andrews, Evan (31 December 2012). “5 Ancient New Year’s Celebrations” History News. Retrieved 31 January 2014).

Kalenda ya mwanzo ya dola la Roma iliweka Machi 1 kama siku ya mwaka mpya, kwa sababu katika ufalme wa Roma walikuwa na Kalenda yenye miezi 10 tu, ikianzia Machi hadi Disemba, hivyo mwaka mpya ulikuwa katika mwezi Machi ambao ulikuwa ni mwezi wa kwanza. Mwezi Machi unathibitishwa pia kwa majina ya miezi mingine iliyofuata kuwa ulikuwa ni mwezi wa kwanza kwa sababu mwezi Septemba hadi Disemba katika kilatini ni majina ya “namba”. Kwa mfano; (septem kwa kilatini ni “saba,” octo ni “nane,” novem ni “tisa,” na decem ni “kumi.”); hivyo Disemba ilikuwa ni mwezi wa 10 na Machi ilikuwa mwezi wa kwanza, jumla miezi 10 ya kalenda ya kwanza ya Roma.

Je “Januari” iliingiliaje katika miezi hiyo na kuwa mwezi wa kwanza?

Mahali pa kwanza na Mara ya kwanza ambapo mwaka mpya ulisherekewa katika Januari 1 ilikuwa ni huko Roma mnamo mwaka 153 KK. Hata hivyo, mwezi Januari awali haukuwepo mpaka mwaka 700 KK, ambapo mfalme wa pili wa Roma, Numa Pontilius, aliiongeza miezi, wa Januari na wa Februari katika Kalenda ya Roma. Kwa sababu hiyo mwaka mpya ulihamishwa kutoka Machi 1 na ukawekwa Januari 1, kwa maana Januari ndio ulikuwa mwanzo wa mwaka katika serikali. Hata hivyo januari 1 haikujulikana sehemu kubwa, na hivyo wakati mwingine Machi 1 iliendelea kuadhimishwa kama mwaka mpya.

Sababu kuu kwanini mfalme wa pili wa dola la Roma, Numa Pontilius, aliweka Januari 1 kama mwaka mpya; inaaminika kuwa jina Januari lilitokana na jina la mungu wa Roma mwenye vichwa viwili aliyeitwa “Janus”. mungu huyo alikuwa ni mungu wa “milango” na “mianzo” n.k. Hivyo mfalme Numa Pontilius aliona ni vema kuiweka Januari 1 kama siku ya sherehe ya mwaka mpya na ibaada kwa ajili ya mungu Janus.

Kwakuwa mungu Janus alikuwa mungu wa milango na mianzo, hivyo waliamini kwamba kwa kumfanyia ibaada za sherehe mwanzoni mwa mwaka; angeliwafungulia milango ya baraka kwa mwaka huo wote, na angelianzisha mwaka wenye heri. Hivyo watu walitakiana “heri ya mwaka mpya” (happy new year) wakiamini kwamba mungu wao wanayempa ibaada siku hiyo angewajalia mwaka wenye heri. Hii ni ibaada ya kipagani na haipaswi Mkristo yeyote mwaminifu akamatwe katika mtego huu wa kusherekea mwaka mpya tena katika siku ileile ya Januari 1.

Katika mwaka 46 KK mfalme Julius Caesar akitawala juu ya ufalme wa Roma alifanya mabadiliko kidogo katika kalenda ya serikali ya Roma, kalenda yake hasa ilianza mwaka 153 KK ambapo Januari 1 ilithaminiwa sana na kuendelezwa kama siku ya mwaka mpya, inaaminika kwamba; ni kwa sababu ya mungu Janus ndio maana Waroma walipendezwa sana kwamba mwezi Januari uwe mwanzo wa mwaka; kwa maana jina lake linatokana na jina la mungu Janus.

Baada ya mfalme Julius Caesar mwaka 46 KK kuifanyia matengenezo kalenda kama “Kalenda ya Julio” (Julian Calendar), alimwua barozi wake kwa sababu alikuwa amependekeza kumwabudu mfalme siku ya Januri 1, 42 KK, katika kuheshimu maisha yake na kuheshimu uanzishaji wa kalenda yake mpya. (rejea; Warrior, Valerie (2006). Roman Religion. Cambridge University Press. p. 110.; Courtney, G.Et tu Judas, then fall Jesus (iUniverse, Inc 1992), p. 50.)

Katika mwaka 567 BK Baraza la Tours liliivunja January 1 kama siku ya mwanzo wa mwaka. Katika nyakati mbalimbali na maeneo mbalimbali pote katika Ukristo wa Ulaya, siku ya mwaka mpya iliadhimishwa katika Disemba 25, na kuzaliwa kwa Yesu kuliadhimishwa katika Machi 1.

“Miongoni mwa wapagani wa karne ya 7 wa Flanders na Netherlands, ilikuwa ni desturi kupeana zawadi katika siku ya mwaka mpya.” -(Wikipedia the free Encyclopedia, “New Year’s Day”)

Januari 1 ikalejeshwa upy

a na kanisa Katoliki.

Katika mwaka 1582 utengenezwaji wa kalenda ya Papa Gregorio, uliirudisha Januari 1 kama siku ya mwaka mpya. Baadaye mataifa mengi na koloni nyingi zilianza kutumia kalenda hiyo ya Gregorio. Hadi hivi sasa ni nchi chache tu ambazo husherekea mwaka mpya katika siku tofauti na Januari 1, lakini nchi zote zinazotumia kalenda ya Gregorio husherekea mwaka mpya katika Januari 1 siku ambayo inaaminika ilikuwa maalumu kwa ajili ya mungu Janus.