Jump to content

User:Urafiki

From Wikipedia, the free encyclopedia

WIKIPEDIA, KAMUSI ELEZO HURU

Chuo kikuu cha urafiki wa watu cha Urusi- Ni moja kati ya vyuo vikuu vinavyoongoza nchini Urusi kwa utoaji elimu bora na chenye hadhi kwenye shirikisho. Chuo kikuu cha urafiki wa watu cha Urusi kilianzishwa na imara amri ya baraza la mawaziri la umoja wa kisovieti mnamo Februari 5 1960. Tarehe 5 mwezi Februari 1992, serikali ya shirikisho ya Urusi iliamua kubadii jina la chuo hicho na kukiita ‘Chuo cha Urafiki wa Watu cha Urusi’. Kuanzia mwaka 1961 hadi 1992 Chuo cha Urafiki wa Watu cha Urusi kilipewa jina la Chuo Kikuu Cha Patrice Lumumba. Uwezo na sifa ya Chuo Kikuu cha Urafiki wa watu cha Urusi kimataifa: Miongoni mwa wanafunzi wa shahada ya kwanza,shahada ya pili na ya tatu ni wawakilishi wa makabila zaidi ya 450 kutoka zaidi ya nchi 146 duniani. Kwenye vikundi vya mafunzo na kwenye vyumba mabwenini kunazingatiwa kanuni za kimataifa, ikiwa ni kuishi na kujifunza kwa pamoja kwa wanafunzi wote toka nchi mbalimbali duniani. Chuo kikuu cha Urafiki wa watu cha Urusi kina takribani jumla ya wanafunzi 25000 wanaochukua shahada ya kwanza, shahada ya pili na shahada ya tatu. Mkuu wa chuo kikuu kwa sasa ni mheshimiwa Vladimir Mihailovich Filippov ambaye alikua waziri wa elimu wa serikali ya shirikisho la Urusi kuanzia mwaka 1998 hadi 2004. Historia ya chuo kikuu cha Urafiki wa Watu cha Urusi Uanzishwaji wa chuo kikuu cha Urafiki kilichopewa jina la Patrice Lumumba. Uamuzi juu ya uwanzishwaji wa chuo kikuu cha Urafiki katika umoja wa kisovieti ulikua ni kutokana na mahitaji ya kutoa msaada wa kiutamaduni katika nchi mbalimbali zilizokua zikitawaliwa na wakoloni ili kupata uhuru wao kutoka katika utawala wa kikoloni mnamo miaka ya 1950 hadi 1960. Kazi kubwa ya chuo kikuu cha Urafiki ilikua ni kuwaandaa wahitimu kuwa wafanyakazi wenye sifa ya juu kwa ajiri ya nchi za mabara ya Asia, Afrika na Amerika ya kusini na kuleta roho ya urafiki kati ya watu hao. Aidha chuo kikuu cha Urafiki kilitoa na kinaendelea kinatoa fursa ya kuendeleza elimu ya juu kwa vijana kutoka katika familia zenye kipato cha chini. Usaili wa wanafunzi ulifanyika kupitia mashirika ya jamii(mashirika yasio ya kiserikali), mashirika ya serikali na siku zilizofuata ulifanyika pia kupitia balozi za umoja wa kisovieti. Waasisi wa chuo kikuu cha Urafiki ni Umoja wa baraza la wafanya kazi, Kamati ya kisovieti ya Ushikiano wa nchi kutoka bara la Asia na Afrika, Umoja wa vyama vya mahusiano ya kirafiki na utamaduni na nchi za nje wa Urusi. Mwaka 1961 chuo kilipewa jina la Patrice Lumumba kama heshima kwake. Patrice Lumumba alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo, mmoja wa kioo cha jamii katika harakati za taifa na katika ukombozi wa watu wa Afrika. Masoma katika chuo kikuu cha Urafiki wa Watu yalianza rasmi mwaka 1960 katika kitivo cha maandalizi ya Lugha ya kirusi na mwaka 1961 katika vitivo vya Uhandisi, Filolojia, sayansi ya udaktari , kilimo, fizikia-hisabati na sayansi asilia, Uchumi na sheria. Wataalam 288 kutoka nchi 47 duniani waliitimu kwa mara ya kwanza mwaka 1965. Mwaka 1964 Chuo kikuu cha urafiki kilikubaliwa kuwa mwanachama wa shirikisho la kimataifa la vyuo vikuu(IAU) na kupata uwezo wa kutuma maafisa wawakilishi katika sikukuu ya festivali ya dunia ya vijana na wanafunzi. Mwaka 1975 chuo kikuu cha urafiki wa Watu kilitunukiwa tuzo ya ‘Urafiki kwa Watu’ kwa mchango wake mkubwa wa kutoa elimu na mafunzo na kuwaandaa wataalam kwa ajiri ya nchi kutoka mabara ya Asia, Afrika na Amerika ya kusini.

Chuo cha urafiki wa watu jn. Patrice Lumumba – Chuo cha urafiki wa watu cha Urusi Mnamo Februari 5 mwaka 1992 utaratibu wa serikali ya shirikisho la Urusi namba 229, ulikibadili jina chuo hicho na kukiita Chuo kikuu cha Urafiki wa Watu cha Urusi. Hivyo mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu cha Urisi ni Serikali ya shirikisho la Urusi. Mnamo miaka ya 1990 chuo kilifungua vitivyo vipya(Mazingira, uchumi, sheria, Filolojia, sayansi ya jamii, maendeleo ya taaluma ya ualimu wa Lugha ya kirusi kama lugha ya kigeni, elimu ya tiba endelevu kwa wafanyakazi, taasisi ya elimu ya lugha za kigeni, uchumi wa kimataifa na bishara, elimu ya mbali, ukarimu na utalii, gravitia na kosmolojia), uliundwa mfumo wa elimu ya maandalizi kabla ya kuanza chuo kikuu kwa kitivo husika na elimu ya ziada. Kwa sasa chuo kikuu cha Urafiki wa watu kimejikita katika mifumo miwili sawia ya utoaji elimu:kwa shahada ya kwanza na shahada ya pili. Mwaka 2000 katika chuo cha urafiki wa watu ilifunguliwa idara ya “UNESCO”(Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulika na elimu, sayansi na utamaduni)-lenye sera ya elimu linganishi. Siku hizi wahitimu kutoka katika chuo cha urafiki wa watu wanafanya kazi katika zaidi ya nchi 170 duniani na kuchangia ushirikiano baina ya nchi hizo na Urusi.

VITIVO NA TAASISI ZA KITAALUMA Kwenye Chuo kikuu cha Urafiki wa Watu cha Urusi katika wigo wa elimu na sayansi kuna vitivo 10 muhimu ambavo ni (sayansi ya kilimo, sayansi ya jamii, uhandisi, udaktari, lugha ya kirusi na masomo kwa ujumla, Fizikia-Hisabati na sayansi asilia, filolojia, mazingira, uchumi na sheria), matawi 3 muhimu kwa ajili ya kuongeza elimu, idara 3 za ujumla za chuo, taasisi 7,vituo 33 kwa ajili ya utafiti wa elimu, maabara zaidi ya 150 na vituo vya utafiti wa kitaaluma na kisayansi. VITIVO • Kitivo cha Fizikia-Hisabati na sayansi asilia • Kitivo cha tiba(Udaktari) • Kitivo cha kilimo • Kitivo cha Elimu ya Mazingira • Kitivo cha sayansi ya jamii na utu • Kitivo cha Uhandisi • Kitivo cha Filolojia • Kitivo cha Uchumi • Kitivo cha Lugha ya Kirusi na masomo kwa ujumla • Kitivo cha sheria

TAASISI • Taasisi ya lugha za kigeni • Taasisi ya ukarimu na utalii • Taasisi ya mipango ya kimataifa • Taasisi ya uchumi wa dunia na biashara • Taasisi ya utafiti wa elimu ya Gravitia na kosmolojia • Taasisi ya kuendeleza taaluma ya elimu

Idara za Jumla za chuo kikuu Cha Urafiki • Idara ya sera ya elimu Linganishi • Idara ya Elimu ya Michezo na kujenga mwili

VITUO VYA UTAFITI WA KISAYANSI na VITUO KWA AJIRI YA KUENDELEZA TAALUMA YA ELIMU • Vituo vya utafiti wa kisayansi Chuo kikuu cha Urafiki wa Watu cha Urusi kina vituo 40 vya utafiti wa kisayansi. • Vituo kwa ajiri ya kuendeleza taaluma ya elimu Chuo kikuu cha urafiki wa watu cha Urusi kina vituo 28 kwa ajili ya elimu ya ziada, vituo vya mafunzo na utafiti wa taaluma ya elimu ya ziada, na vituo vya kukuza na kuongea taaluma na ujuzi.

Matawi ya Chuo Matawi ya chuo kikuu cha Urafiki wa watu cha Urusi yapo katika miji ifuatayo • Mji wa Sochi ya Krasnodari Krai • Mji wa Yakutsk jamhuri ya Sakha(Yakutia) • Mji wa Yessentuki • Mji wa Belgorod • Mji wa Stavropol • Mji wa Perm

Wakuu wa chuo Chuo kikuu cha Urafiki wa watu cha Urusi • 1960 - 1970 - Sergei Rumyantsev (Julai 18 1913 - 1990) • 1970 - 1993 - Vladimir Stanis (1924 - 2003) • 1993 - 1998 – Vladimir Filippov (kuzaliwa 1951) • 1998 – 2005 – Dmitrii Bilibin (kuzaliwa 1937, mwaka 2004 – 2005 alikua mkuu wa chuo kwa mda. Mkuu wa chuo kuanzia 1998 - 2004 ) • 2005 - Vladimir Filippov (Alichaguliwa tena mwaka 2005)

Miradi ya elimu na Mipango ya chuo Mnamo mwaka 2007 mpango wa elimu wa chuo cha Urafiki wa watu cha Urusi ulikua << kujenga wigo mpana wa ubunifu katika mipango ya elimu na kujenga mazingira ya ubunifu ambayo lengo lake ni kutekeleza maslahi ya taifa la shirikisho la Urusi kupitia mapato yatokanayo na huduma ya elimu >> Kupokea msaada kutoka wizara ya elimu na sayansi ya serikali ya shirikisho la Urusi kwa kuupa kipaumbele mradi wa taifa wa Elimu. Katika mwaka wa masomo 2011 – 2012 miradi 9 ya elimu katika chuo kikuu cha Urafiki cha Urusi ilishinda katika kashindano ya <<Ubunifu juu ya mipango bora ya Elimu Urusi>> miongoni mwake ni Hisabati, Hisabati na sayansi ya compyuta, teknolojia ya habari, matumizi ya Hisabati na sayansi ya kompyuta, sheria, ushirikiano wa kimataifa na Uchumi. Mwaka 2012 kulingana na amri ya Raisi wa serikali ya shirikisho la Urusi namba 293 ya machi 12, 2012, Chuo cha Urafiki wa Watu cha Urusi, Chuo Cha Taifa cha Mosko(Moscow State University) na chuo kikuu cha mji wa St. Petersbag vilipewa uwezo wa kujiendesha vyenyewe na kuendeleza miradi yake ya Elimu na kufuatilia utekelezaje wake. Kazi za Kisayansi Takribani wafanyakazi 500 wa chuo kikuu cha Urafiki ni wavumbuzi na wagunduzi wa kisayansi. Katika msingi wa mweledi kwenye chuo kikuu cha Urafiki wa watu cha Urusi kinajumuisha takribani hati miliki 870 na leseni 150 za shirikisho la Urusi kwa upande wa shughuli za kisayansi za chuo. Chuo kikuu cha Urafiki wa Watu cha Urusi kinashiriki katika utekelezaji wa miradi ya utafiti kwa kuwa na kipaumbele katika masuala ya utafiti, ikiwa ni amri ya makampuni ya Urusi na ya nchi za nje. Mnamo mwaka 2010 umoja wa kibiashara ujulikanao kama Amerikano-Rasiskii(Amerikano-Urusi) ulikitunuku chuo medali ya dhahabu ya << Innoviations for Investments to the future>>maana nake ‘Ubunifu kwa uwekezaji wa maisha ya baadae’ kwa ubunifu wake ulioufanya. Kazi ya utafiti wa kisayansi mnamo mwaka 2011 ulifanyika chini ya mipango ya shirikisho zifuatazo: << Sayansi na ufundishaji sayansi bunifu kwa wafanyakazi wa Urusi, >>, << shirikisho la Lugha ya kirusi>>, <<utafiti na maendeleo yenye kipaumbele katika nyanja za kisayansi na teknolojia nchini Urusi kuanzia mwaka 2007 - 2013 >>, Uchambuzi <<Maendeleo ya kisayansi kwenye elimu ya juu>> na kadhalika. Mwaka 2011 chuo kikuu kilikua moja ya washindi wa mikakati ya kukuza maendeleo ya vyuo vikuu vya serikali kwa kuboresha usimamizi wa taasisi za elimu ya juu , pia usawazisho wa maudhui na muundo wa elimu, mahitaji ya soko la ajira, na mikakati ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi. Mwaka 2011 chuo cha Urafiki wa Watu cha Urusi kilichukua nafasi ya kwanza kwenye gredi ya taifa ya vyuo vikuu kwenye shughuli za kimataifa.

Bulletini ya Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu cha Urusi Bulletini ilichapishwa na chuo kikuu cha urafiki wa watu cha Urusi. Uchapishwaji una mifululizo 32. Kampasi ya Chuo Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu kina kampasi yake katika mtaa wa Miklukho- Maklaya, yenye majengo ambayo huishi wanafunzi zaidi ya 7,000 wa shahada ya kwanza,shahada ya pili na shahada ya tatu. Kwenye kampasi ya chuo mtaa huo huo wa Miklukho-Maklaya kuna: • Jengo kuu la utawala(Kresi)(Hapo kuna ofisi ya mkuu wa chuo, huduma za chuo namashirika, vitivyo vya sheria, Filolojia, uchumi, biashara ya kimataifa) • Jengo la kitivo cha kilimo • Jengo la kitivo cha tiba(Udaktari) • Jingo la kitivo cha maandalizi ya mwaka wa lugha ya kirusi • Jengola kitivo cha sayansi jamii na utu • Jingo la Achivu • Jingo la mazoezi ya mwili kwa afya(Fitness Center), viwanja 4 vya mpira wa miguu, viwanja 6 vya nje na 9 vya ndani vya tenesi. • Kliniki namba 25 na kituo cha afya cha chuo cha Urafiki • Kituo cha kimataifa cha utamaduni (InterClub) • Kefu za mtandao(Internet Cafes) • Migahawa yenye mapishi mblimbali asilia, mesi za wanafunzi • Maduka kwenye kila bweni • Kituo cha polisi kwa ajiri ya chuo kikuu cha Urafiki wa Watu cha Urusi.

Vitivo vya uhandisi, Fizikia-Hisabati na sayansi asilia vipo katika mtaa wa Ordzhonikidze; Kitivo cha mazingira kipo mtaa wa Podolskom Shosse. Mabweni ya chuo kikuu yalipewa hadhi ya ubora mwaka 2011 kwa matokeo ya mashindano ya <<Nyumba ya wanafunzi wetu>> yaliofanywa na sera ya mji wa Mosko ya idara ya familia na vijana.