User:Tz.mzawa
HISTORIA YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF TULIYEMZIKA LEO HAPA LINDI JINA: Abdallah Seif Linganaweka KUZALIWA : 1939, Kijiji Cha Dimba SEHEMU YA KUZALIWA : Kijiji Cha Dimba, Lindi. KUFARIKI: 12/09/2020 – Nyumbani kwake Chamazi
Mpaka umauti unamkuta Sheikh Abdallah Seif Ling’anaweka alikua ndio sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Mashia Tanzania inayotambulika kwa jina la Tanzania Ithna Ashariyyah Community yenye makao yake makuu Kigogo Post, Kinondoni – Dar es Salaam Tanzania.
Sheikh Abdallah Seif ni miongoni mwa wasomi wazawa wa mwanzo kabisa wa kishia Tanzania aliyepata elimu yake ndani nan je ya nchi, Walimu wake waliomfundisha nje ya nchi akiwa Iraq, Iran na Lebanon ni Ayatollah Sayyed Baqir Sadr, Ayatollah Sayyid Muhsin Alhakim, Sayyed Mussa Sadr na wengine.
Miongoni mwa walimu wake wa mwanzo ni Sayyid Akhtar Rizvi mmoja wa wanazuoni walioasisi taasisi ya Bilal Tanzania – Mwaka 1968 Sheikh Abdallah alisafiri kwa mara ya kwanza kwa usafiri wa maji mpaka mji wa Iraq kwaajili ya kujiendeleza kwa masomo ya juu.
Sheikh Abdallah seif ni mmoja wa waasisi wa harakati za kufundisha dini ya Kiislamu na madhehebu ya Ahlulbayt huko Mozambique na mpaka anafariki alikua akiendesha chou binafsi cha dini katika Kijiji chake cha Mnang’ole ambapo kuna huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo kusambaza maji katika maeneo yenye uhaba.