User:Nurdin mataka
NURDIN MATAKA
(The conscious Nuyama)
NURDIN(Nuyama) ni mtoto wa5 kuzaliwa kati ya watoto7 katika familia ya mzee/mwalimu/Alhaji MATAKA na mama Mataka, Familia hiyo inayotokana na ukoo wa kisultani(ki-chief, mwenye MATAKA) yenye watoto 6 wakiume na 1 wakike ambae kazaliwa baada ya kuzaliwa Nuyama. Nao ni 1-Jafari, 2-Hamisi, 3-Hamza, Hamadi, 5-Nudini(Nuyama) ,6-Sofia, 7-Yunusi
Nurdin alipatiwa jina la utani au jina la ziada(Nick name) inayofahamika kama NUYAMA akiwa na miaka 10 na alipewa jina hilo na kaka yake watatu kuzaliwa anayeitwa Hamza na kujiita HAYAMA, jina hilo la Nuyama limetokana na majina yake matatu yani Nurdin(NU) Yasin(YA) Mataka(MA)= NUYAMA. Lililoanza kufahamika zaidi miaka ya2004 na kupata umaarufu miaka ya 2006.
Nuyama kazaliwa 17/12/1990 katika hospitali ya wilaya ya Tunduru iliyopo mkoa wa Ruvuma(TANZANIA) na aliishi na kukulia Tunduru, alianza darasa la awali(miaka hiyo chekechea) 1997 katika shule ya msingi Majengo iliyopo wilayani Tunduru mjini lakini alishindwa kuendelea na darasa la kwanza mwaka ulofuatia kutokana na kuonesha tabia za fujo na utukutu jambo lililopelekea ashindwe kuweka umakini kwenye masomo hivyo baba yake (Mwalimu mataka) aliyekuwa mwalimu shuleni hapo miaka hiyo kuamua kumsitisha asiendelee na darasa linalofuata hadi atapotulia au kupunguza fujo na utukutu, jambo hilo lilipelekea asome awali(chekechea) kwa miaka miwili hadi 1999 alipoanza darasa la kwanza rasmi na kuhitimu elimu ya darasa la saba mwaka 2005.
Mwaka 2006 alifaulu na kuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya kutwa ya Frank-weston iliyopo Tunduru mjini, ilipofika mwaka2008 akiwa kidato cha tatu alisimamishwa shule na kufukuzwa na bodi ya shule kutokana na tabia zake za utukutu,ugomvi na ubabe kwa wanafunzi wenzake, walimu na hata raia wa kawaida mitaani. Kutokana na kupenda kufanya mazoezi ya kunyanyua vyuma vizito na mapigano ilimfanya awe sugu na mpenda mapigano wakati wote jambo lililopelekea karibu kila siku apate kesi za kupiga watu wa rika mbalimbali (moja ya sifa yake kubwa ni mtu anayejiamini na kujikubali) hali ilosababisha kupata wafuasi wengi vijana watukutu wapenda ugomvi na fujo. moja kati ya mambo ambayo hajawahi kuyafanya ingawa watu hawakuwahi kuamini ni kwamba pamoja na utukutu na fujo zote hakuwahi na hajawahi kutumia kilevi chochote iwe kuvuta sigara au bangi wala kuywa pombe.
Mwaka huo wa 2008 mwezi wa9 akahamishiwa katika shule binafsi ya sekondari ya Taifa foundation iliyokuwa chini ya masister wakihindi wa DMI(daughter of marry imaculate) iliyopo manispaa ya songea Ruhuwiko njia ya kwenda airport ambayo ni makao makuu ya mkoa wa ruvuma lakini ilihamishiwa mshangano hapohapo songea hilo lilikuwa jepesi kwasababu wazazi wake wote walikuwa ni watumishi(wafanyakazi) wa serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania hivyo suala la kipato hakikuwa kikwazo kwao, alisoma vizuri na alitulia baada ya ndugu, jamaa na marafiki ikiwemo wazazi kumuasa aache fujo na utukutu kwa mustakabali bora wa maisha yake na hilo likawezekana na kufanikiwa kwa90% na kuzaa matunda yalopelekea kufanikiwa kuhitimu elimu ya sekondari ya kidato cha Nne mwaka2009.
Hadi anahitimu elimu ya sekondari alikuwa bado mazoezi ya mapigano anaendelea kufanya ingawa hakuwa mtukutu na mgomvi tena hiyo ilitokana na ukuaji wa umri na utambuzi wa kifikra na ugeni wa mazingira yale alopelekwa.
2010 alijiunga na chuo cha kati(college) kilichokuwa kinaitwa SLADS- school of library archives and documentation studies kilichopo Bagamoyo ambako alisoma ngazi ya cheti(certificate) hadi2011 alipomaliza ngazi hiyo. Mwaka 2012 alijiunga na jeshi la kujenga Taifa(JKT) KJ-148 mafinga kwa muda wa miezi 7 ya mafunzo na kwa bahati baada ya kumaliza mafunzo akachaguliwa kujiunga na Jeshi la wanainchi wa Tanzania(JWTZ) kikosi cha mizinga morogoro, hata hivyo huko hakudumu na mzimu wake wa mapigano ulimfuata na kusababisha afukuzwe jeshi-5/11/2012 baada ya MP(military police) kambini hapo kuja kutuluza fujo na kutoa adhabu kwa kikosi ambacho kilihusika na fujo hizo bila kujali nani alikuwepo na nani hakuwepo kama sheria na kanuni za kijeshi zisemavyo lakini Nuyama alikataa kwakuwa wakati wa tukio hakuwepo hali ilopelekea kuanza kuvutana na kusababisha Nuyama awapige kisawasawa maafande hao waliokuwa kama12 wenye vyeo vya makoplo na makepteni 3, Tukio hilo lilisababisha awavunje mikono,miguu na viuno maaskari hao walomzidi umri,vyeo na wadhifa na kusababisha afungwe kwenye jelamaalumu kwa watu maalum na hatari ya kijeshi kwa mda wa miezi 6 na baada ya kutoka akafukuzwa jeshini (ingawa alifukuzwa lakini alikuwa ni askari shupavu na mkakamavu asieogopa wala kutishika na hata kuyumbishwa na chochote na hiyo ni kutokana na maisha yake ya nyuma na tabia yake ya kupenda mazoezi na kujiamini sana, Na yeye ni kati ya maaskari waliofuzu vizuri kozi ya ulengaji(udunguaji-sniper) kwa kupiga risasi 198 kati ya200 akikosa 2tu kwa umbali na mikao tofautitofauti.
Mwaka2013 mwezi wa8 alijiunga na chuo cha kati(college) kinachoitwa ST.joseph college(chuo cha mtakatifu josephu kilikuwepo morogoro kihonda kwa wakati huo sasa kipo mzani barabara ya kwenda dodoma hapohapo morogoro, alijiunga na kozi ya IT(Information technology) kwa ngazi ya diploma na alisoma kwa miaka miaka miliwi hadi mwaka2015 mwezi wa5 alipohitimu na kujiunga na Kikosi maalumu na cha siri cha ulinzi waTaifa kilichopo chini ya idara ya usalama wa Taifa kiitwacho kikosi Namba5 ambacho alikitumikia kwa karibu, utii, nidhamu,kwa kujituma na usiri wa hali ya juu hadi mwaka 2017 alipobadilishiwa majukumu na kuanza kuonekana tena mtaani na vijiweni.
kuanzia mwaka 2018 amekuwa ni mtu wa watu sio yule nuyama katiri sura mbuzi asiye cheka na watu, saivi ni kipenzi cha watu na ni kipezi cha watu na mtu wakujitoa katika mambo mbalimbali kama ya kijamii na yale ya binafsi pia amekuwa mkulima wa mahindi na korosho lakini bila kusahau ni mjasiliamali wa vitu na biashara ndogondogo.
katika safari yake ya maisha ya mahusiano ya kimapenzi amedate na wasichana kadhaa na kufanikiwa kupata mtoto mmoja kwa msichana mmoja kati ya hao na huyo mtoto ni wakiume aitwa Nurdin(NUYAMA Jr) karithi jina la baba yake.
Mwaka 2019 aliingia rasmi kwenye mambo ya siasa na kujiunga na chama cha mapinduzi CCM ambapo alichaguliwa kuwa kiongozi wa umoja wa vijana ktk kitongoji chao na baadae kuwa mjumbe wa kamati ya siasa ya UVCCM kata ya Majengo. Ni mpenzi sana wa kufuatilia mambo mbalimbali kama yakitafiti,harakati,kichambuzi na siasa za kimataifa hasa za bara la asia(North korea, Russia, China) na-Cuba, venezuela kwa upande wa magharibi. Tanzania na mataifa mengine ya kikomunist(communist) na kisoshalist(socialist) lakini pia siasa za kibepari ingawa kwa uchache kama america, england, germany, italy na france. lakini pia ni mfuasi wa siasa za mwalimu nyerere, fid el castro, che guevara, magufuli na chief mataka.
2020 amekuwa mstari wa mbele kutangaza sera za chama cha mapinduzi akiwa na rafiki zake wa karibu na kuwashawishi watu kujiunga na chama hicho mama na chenye malengo na mustakabali bora kwa Taifa la TANZANIA.
Mwaka 2022 mwezi7 katika uchaguzi wa ndani wa uongozi chama cha mapinduzi katika nafasi ya ukatibu kata wa kata ya MAJENGO iliyopo wilayani TUNDURU mkoani RUVUMA TANZANIA Nuyama anafanikiwa kushinda kwenye uchaguzi na kushika nafasi hiyo ambayo atahudumu nayo hadi 2027 utapofanyika uchaguzi mwingine.
MWENYEZI MUNGU
ibariki TANZANIA
Iibariki AFRIKA
ibariki DUNIA
m'bariki NUYAMA na WATANZANIA WOTE.