Jump to content

User:Kivisamedia

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ziwa kingili Ni miongoni mwa maziwa mazuri yenye mvuto wa kipekee Nchini Tanzania, ziwa kingili ni ziwa linalo patikana mkoani mbeya katika wilaya za Kyela na Busokelo Ziwa ambalo asili yake ni mlipuko wa Volkano Ndio maana kitalaamu linajulikana kama KINGILI CRATER LAKE.

Muonekano wa kuvutia wa Ziwa hili kwanzia maji yake mpaka mazingira yanayo lizunguka ziwa hili ndio upekee unao lifanya ziwa hili liwe tafauti na maziwa mengine nchini Tanzania.

Ziwa Kingili linezungukwa na Uoto wa asili ambao in misitu myepesi myepesi inayo kaliwa na Tumbili wa Kijivu,Ndege wa kila aina pamoja na wanyama kadha wa kadha wanao zidi kulipamba ziwa hili.

Ziwa Kingili ni ziwa linalopatika karibu ama katikati ya makazi ya watu ambao ni wakazi wa kijiji cha Kingili kwa upande wa kusini na kijiji cha Mpunguti au Ntaba kwa upande wa Kaskazini.

Wakazi wa Eneo hili ni Watu wa kabila la Kinyakyusa miongoni mwa makabila maarufu sana nchini Tanzania.

wakazi wa Eneo hili hutegemeo maji ya Ziwa hili kwa asilimi 98% katika shughuli zao za kila siku na hasa kwa matumizi ya majumbani.

Ziwa Kingili linasifika kwa kuwa na maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu jambo ambalo ni tafauti na maziwa mengine.

Maji ya ziwa Kingili ni meupe jambo ambalo linamfanya mtu kuweza mchanga pamoja na samaki ndani ya maji hadi urefu wa kina cha mita mbili(2M).

Ziwa Kingili linasifika kwa kuwa na maji ya Uvugu vugu Nyakati za Jioni,usiku hadi Asubuhi na kuwa na maji ya ubaridi kiasi katika nyakati za mchana.

Moja kati ya vuvutio maarufu sana katika ziwa Kingili ni pamoja na Jiwe kubwa lenye RANGI YA CHUNGWA linalopatika upande wa kusini magharibi mwa ziwa.

Ziwa Kingili ni ziwa ambalo halina rekodi ya kuwa na wanyama wakali kama Mamba na kadhalika.

Kina cha ziwa Kingili huongezeka katika kipindi cha mvua zinazo nyesha kwanzia mwezi wa February hadi mwezi May,na kina kupungua katika kipindi cha Kiangazi kwanzia mwezi July mpaka mwezi wa January.