Jump to content

User:Elia Kikoti

From Wikipedia, the free encyclopedia

Michezo ya mahasimu "Derby"

[edit]

Neno "michezo ya mahasimu" kwa kingereza "Derby" neno hili lililokopwa kutoka Kiingereza. Historia ya "derby" au "mechi za derby" katika mpira wa miguu. Mechi ya kwanza kabisa ya derby ambayo neno "derby" linahusishwa nayo ilikuwa nchini Uingereza kati ya timu mbili za mji wa Sheffield. Hapo awali jina "Derby" lilitolewa kwenye jina la Lord Stanley of Derby ambaye alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliohudhuria mchezo huo kati ya Sheffield F.C. and Hallam F.C. Kwa muda, neno "derby" likaanza kutumika kuelezea mechi yoyote kati ya timu hasama kutoka eneo moja.Munamo karne ya 19 nchini Uingereza neno "Derby" lilianza kutumika.
Hivyo kutokana na michezo ya mahasimu “Derby” kuhusisha timu hasama toka eneo moja jambo hili limeongeza utani wa jadi, Imani,ushindani na kukua kwa soka kwa vilabu pinzani duniani kote .Katika kukua huko kumesababisha vilabu hivyo kujipatia fedha na mapato makubwa katika uazaji wa jezi /fulana , mapato ya viingilio , paomja na pesa kutoka kwa wadhamini. Michezo hii ya mahasimu “Derby” imefanya vijana wengi kupendezwa na kuwa na ndoto za kuja kuchezea timu hizo kutokana na ushawishi wa mashabiki ambao timu hizo zimebeba katika soka .Jambo hili limefanya soka kukua kwa kiasi kikubwa kwani upinzani unarisishwa vizazi na vizazi.

MIONGONI MWA “DERBY” KUBWA BARANI AFRIKA

[edit]

1. Cairo Derby -Al-ahly vs Zamalek(Misri)

Hii unaweza kusema ndio Derby bora zaidi barani Afrika ambayo imechezwa tangua karne ua 19 hadi hii leo. Al ahly vs Zamalek ni timu zinazotoka jiji la Cairo ni vilabu kongwe vilivyoanzishwa mwanzoni mwa karne ya 19. Huku Al-ahly ikianzishwa mwaka 1907 na miaka minne baadaye nao Zamalek wakiazisha timu yao na kila timu ina rekodi zake dhidi ya mwenzake na ndio maana shirikisho la soka Afrika (CAF) Walizitambua timu hizi ni vilabu bora vya karne ya 20C kwani upinzani wa ndani na nje ya soka baina ya timu hizi mbili umeziwezesha vilabu hivi kuweza kupata makombe mbalimbali ndani ya misri hata kwa mashindano ya nje .
Kwani munamo 2019-2020 katika mashindano ya CAF kwa ngazi ya vilabu timu hizi mbili ziliweza fika fainali zote kwa Pamoja na kufanya kuwa fainali ya kwanza kwa timu za hasimu kwa kupigwa mjini Cairo katika dimba la Cairo stadium November 27,2020 inchini Misri.



2. Soweto Derby-Kaizer Chief vs Orlando Pirates (Afrika Kusini)

Mitaa ya Soweto huwa inachafuka kwa rangi nyeusi na Orange kuashiria timu zao pendwa za mitaa hiyo, ni Kaizer Chief dhidi ya Orlando Pirates ndio wanaiwakilisha Derby kubwa nchini Afrika Kusini.
Derby hiyo imeandikwa kwenye vitabu vya soka kwa kuwa na mvutano na upinzani mkubwa, mara nyingi huchezwa kwenye dimba la FNB Stadium lenye uwezo wa kubeba mashabiki 90,000 kwa pamoja.
Moja ya tukio lisilosahaurika ni vurugu zilizotokea kwenye miaka ya nyuma “The Ellis Park na Orkney Stadium Disaster ambapo vifo takribani 42 vilirekodiwa.


Derby hii ina takribani miaka 40 tangu ianzishwe kwake miaka ya 1970.


3. Tunis Derby-Club Africain vs Esparence (Tunisia)

Timu hizi hazijatofautiana sana kuzaliwa kwakwe ilianza Esparence de Tunis mwaka 1919 ikiwakilisha tabaka la watu wa chini na mwaka uliofuatia 1920 Club Africain ilianzishwa ikiwakilisha tabaka la watu wenye pesa. Kwa miaka mingi sana Esparence amekuwa akionesha kiwango kizuri dhidi ya mpinzani wake kwenye mashindano ya ndani na ya kimataifa. kwa pamoja wanatumia uwanja wa El Menzah au Stade el Menzah wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60.000.

4. Wydad Casablanca vs Raja Casablanca- Casablanca Derby, (Morocco)

Kwa mara ya kwanza timu hizi zilikutana 1956 huku rekodi zikimbeba zaidi Raja Casablanca dhidi ya Wydad Casablanca. Timu hizi zinatumia uwanja wa Mohammed wa V ambapo kwa mara ya kwanza mwaka 2019 timu hizi zilikutana kwenye mashindano ya Arab Club Championship na kuweka rekodi ya miamba hiyo kukutana nje ya mashindano ya ndani.


5. Kariakoo Derby, Simba SC vs Yanga SC (Tanzania)

Timu hizi zote zinapatikana mitaa ya Kariakoo huku Yanga ikianzishwa munamo mwaka 1935 na mwaka mmoja baadaye Simba nayo ikaanzishwa ,lakini kwa sasa makazi yao yamehama mmoja akiwa Oysterbay huku Wananchi wakiweka kambi yao maeneo ya Avic Town Kigamboni japo swala hili halojabadili utani wao wa jadi huku Kariakoo ikitawaliwa na nyekundu/nyeupe na kijani/njano kipindi cha derby.
Derby ya kwanza ya Kariakoo ilichezwa Juni 7,1965 mara baada ya kuanzishwa kwa ligi kuu ya soka .Yanga ilishinda kwa goli 1-0 dhidi ya Sunderland (sasa simba) huku mfungaji wa kwanza akiwa ni Mawazo Shomvi aliyefunga dakika ya 15 Hakuna asiyejua upinzani ndani ya uwanja kwa wachezaji wa timu hizi, na nje ya uwanja kwa mashabiki. Derby hii imeandikisha michezo zaidi ya 100 mpaka sasa tangu kuanzishwa kwake mwaka 1965.


MIONGONI MWA “DERBY” KUBWA BARANI ULAYA

[edit]

1. River Plate vs Boca Juniors- superclásico, (Argentina)
Hii ndiyo Derby nambari moja Duniani kwani Timu hizi zina upizani wa juu ndani na nje ya uwanja jambo lililopelekea hata michezo yao kuchezwa nje ya bara/nchi sababu ya vurugu na ishu za kiusalama.
Vilabu hivi viwili vya Boca na River Plate vyote vina asili katika La Boca, eneo la viwanda la mji wa Buenos Aires, ambapo River ilianzishwa mnamo 1901 na Boca mnamo 1905. Hata hivyo, River, ilihama kwenda eneo tajiri la Núñez kaskazini mwa mji mwaka wa 1925. Tangu wakati huo, Boca Juniors imejulikana kama klabu ya tabaka la wafanyakazi wa Argentina au klabu ya watu, na wafuasi wengi wa Boca wanatoka katika jamii ya wahamiaji wa Kiitaliano wa eneo hilo. Kwa kweli, mashabiki wa Boca wanajulikana kama "Xeneizes" ("Genoese"). Kinyume chake, River Plate ikawa inajulikana kwa jina la utani, Los Millonarios (Mabilionea), ikidhaniwa kuwa na msingi wa msaada wa tabaka la juu. Hata hivyo, vilabu vyote viwili vina wafuasi kutoka katika tabaka zote za kijamii.


Kufikia mwaka wa 1913, vilabu vyote viwili vilikuwa na viwanja vyao La Boca na havikuwa vimepata ubingwa wowote, na pia vilikuwa mbali na umaarufu ambao ungekuja baadaye. Uhasama maarufu zaidi wa soka nchini Argentina hadi wakati huo ulikuwa kati ya Alumni–Belgrano A.C. (vilabu vyote kutoka Belgrano) mpaka Alumni ilivunjika mwaka wa 1911 na Belgrano ikajiondoa kutoka AFA. Racing Club de Avellaneda ilikuwa ya kwanza kati ya Big Five wakati huohuo iliposhinda ubingwa wao wa kwanza wa ligi ambao ulikuwa wa mfululizo wa saba.

2. Real Madrid vs Barcelona -Eclásico, (Hispania)

El Clásico ni zaidi ya mechi ya kawaida ya soka. Ni tukio la kipekee katika ulimwengu wa michezo ambalo huwavutia mamilioni ya watu duniani kote. Kila wanamichezo, wachezaji, na mashabiki wanajua kwamba wanaposhuhudia Real Madrid ikikabiliana na Barcelona, wanashuhudia zaidi ya soka tu - wanashuhudia historia, utamaduni, na migongano ya kisiasa na kitamaduni ya muda mrefu.

Kutoka kwa mtazamo wa michezo, El Clásico inawakutanisha miamba wa soka, Real Madrid na Barcelona, ambao ni miongoni mwa vilabu vikubwa zaidi na vinavyoonekana sana duniani. Kila timu ina historia ndefu ya mafanikio, wachezaji wenye vipaji, na mkondo wa mashabiki wanaojitolea. Kwa wengi, hii ni zaidi ya mechi ya kawaida ya soka; ni shindano kati ya utambulisho wa Kihispania na utambulisho wa Katalunya, ikionyesha mgongano wa kitamaduni kati ya mji mkuu wa Hispania na eneo la Catalonia lenye kujitambulisha.

Mikutano kati ya Real Madrid na Barcelona inahusisha nyota wa mchezo, kama vile Lionel Messi, Cristiano Ronaldo (hapo awali), Sergio Ramos, na wengineo. Wachezaji hawa huongeza uzito na mvuto wa mechi, wakionyesha vipaji vyao bora na kuleta msisimko mkubwa kwa mashabiki.

Lakini El Clásico sio tu juu ya mpira wa miguu. Ni tamasha la utamaduni ambalo linajumuisha hisia za kihistoria na kisiasa za miaka mingi. Kwa wengi, mechi hii inawakilisha zaidi ya matokeo ya mpira wa miguu; inawakilisha ushindani wa kihistoria kati ya pande mbili za Hispania na utambulisho wao wa kipekee.

Rekodi zao za sasa zinaonyesha ushindani mkubwa kati yao. Katika michezo yote, Real Madrid wameshinda mara 97, Barcelona mara 96, na wametoa sare mara 52. Katika La Liga, Real Madrid wameshinda mara 75, Barcelona mara 73, na wametoa sare mara 35. Hizi ni takwimu ambazo zinaonyesha jinsi ushindani huu ni wa karibu sana na ulio na msisimko mkubwa kila wakati wanapokutana.

3. Manchester United vs Manchester City-Manchester Derby, (Uingereza)

Derebi ya Manchester ni mchezo wa mpira wa miguu kati ya Manchester City na Manchester United, ulioanza kuchezwa mwaka 1881. City inacheza kwenye Uwanja wa Etihad huko Bradford, mashariki mwa Manchester, wakati United inacheza kwenye Old Trafford katika mtaa wa Trafford, Greater Manchester; viwanja hivyo viwili vimetenganishwa na umbali wa takriban maili 4. 

Mchezo wa Kwanza: Novemba 12, 1881; St. Mark's (West Gorton) 0–3 Newton Heath LYR

Ushindi Mkubwa: United 1–6 City (1926); United 0–5 City (1955); United 5–0 City (1994); United 1–6 City (2011)
Eneo: Greater Manchester

Fainali ya Kombe la FA ya 2024: Manchester United Yawashinda Manchester City Manchester United walitwaa Kombe la FA msimu wa 2023-24 baada ya kuwashinda wapinzani wao wa jadi, Manchester City, kwa bao 2-1 katika fainali iliyofanyika Uwanja wa Wembley tarehe 9 Mei 2024.

Mchezo:Ilikuwa ni mechi ya kusisimua yenye mashambulizi mengi na nafasi nzuri za kufunga kwa timu zote mbili. Anthony Garnacho alifungua bao la kwanza kwa United dakika ya 30, akimalizia pasi nzuri kutoka kwa Bruno Fernandes. Alejandro Garnacho aliongeza bao la pili dakika ya 39, akipiga shuti kali lililoingia wavuni mwa Ederson Moraes. City walipata bao la kufutia machozi dakika ya 87 kupitia kwa Jeremy Doku, lakini hawakufanikiwa kusawazisha bao. Ushindi huu:
Unaleta taji la 13 la Kombe la FA kwa Manchester United, wakiwa timu ya pili yenye mataji mengi zaidi ya kombe hili nyuma ya Arsenal (14). Unamaliza ukame wa miaka sita wa United bila taji lolote. Unaimarisha uhasama kati ya mashabiki wa timu hizi mbili, na kuifanya Manchester Derby kuwa moto zaidi.