Jump to content

User:Catherine Philipo

From Wikipedia, the free encyclopedia

KIVULI MATATA

[edit]

Pale kijijini Kivulini, kulikuwa na mti mkubwa wa mwembe uitwao "Kivuli Matata" kwa kivuli chake cha giza totoro hata mchana kweupe. Watu walihofia kivuli hiki, wakiamini kinaleta mikosi. Lakini Bwana Tembo, mzee wa kijiji, aliketi chini ya mti huo kila siku bila woga. Kijana mdogo aitwaye Juma alipohoji ujasiri wake, Bwana Tembo alitabasamu na kusema, "Giza ni kivuli tu, sio kikwazo kwa walio na mwanga wa kweli mioyoni mwao." Hapo Juma alielewa kuwa hofu zao zilikuwa ni hadithi tu walizojibebea.

[edit]